Kisomo chatajwa kwa manufaa ya watu na ustawi wa jamii
Na. Muhamad Kulele, DODOMA
Kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje
ya Mfumo Rasmi kimehitimishwa katika viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma,
kwa msisitizo wa kuendeleza maarifa na ujuzi unaogusa maisha ya jamii.
Katika kilele hicho, mgeni rasmi, Katibu Tawala Msaidizi (Elimu), Kiduma Mageni aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati akizungumza na mwanafunzi na mamia ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo alisema kuwa kisomo ni kwa ajili ya manufaa ya watu, jamii na dunia kwa ujumla.
Akiongea katika hotuba iliyobeba taswira na ujumbe kwa
ajili ya kizazi cha leo kujifunza, kushirikiana na kujenga msingi wa kesho iliyo
bora zaidi.
Alisisitiza kuwa elimu yenye maana si ile inayobaki kwenye vitabu pekee, bali ni ile inayogeuka kuwa maarifa, ujuzi, fursa na maendeleo katika jamii.
Comments
Post a Comment