Posts

Makutupora kupata Zahanati Mpya, Mbunge wa Mtumba aweka nguvu kwenye ujenzi

Image
Na. Mwandishi wetu, MAKUTUPORA   Jitihada za kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Mchemwa zimepata nguvu baada ya kuchangiwa matofali 5,000, mifuko 250 ya saruji pamoja na gharama za mafundi hadi hatua ya kufunika jengo, huku wananchi wakihimizwa kushiriki kikamilifu kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika na kuanza kutoa huduma.   Mbunge wa Jimbo la Mtumba Anthony Mavunde alisema kuwa lengo la mchango huo ni kuhakikisha wananchi wa Makutupora wanapata huduma za afya karibu na makazi yao, akisisitiza kuwa ujenzi wa zahanati hiyo haupaswi kuwa jukumu la mtu mmoja, bali ni mradi wa wananchi wote.   “Zahanati si ya kwangu. Zahanati ni ya kwetu. Kila mmoja ahakikishe pale mchanga wake unaingia kwenye zahanati. Naomba mtoe ushirikiano. Kuna baadhi ya gharama si lazima nilipie mimi ila nguvu kazi yenu nayo inaweza kufanikisha jambo hili natamani kuwaona vijana wa hapa wakichapa kazi,” alisema Mavunde.   Mbunge huyo pia alisema kuwa anaamini serikali itaendelea kuu...

Jiji la Dodoma lavuna Tuzo Tano Nanenane, 2026

Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeibuka kidedea katika Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Nanenane Kitaifa 2026 baada ya kutwaa tuzo tano, hatua inayoonesha mafanikio makubwa ya jiji hilo katika kuendeleza sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.   Maonesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela jijini Dodoma na kuhitimishwa Agosti 8, 2026 yaliwakutanisha washiriki mbalimbali kutoka maeneo tofauti ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha ubunifu, teknolojia na fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji.   Katika maonesho hayo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilitwaa nafasi ya kwanza katika makundi ya Kilimo Ndani ya Uwanja, Mifugo Ndani ya Uwanja na Malisho Ndani ya Uwanja kwa upande wa Kanda ya Kati.   Aidha, jiji hilo lilipata nafasi ya pili katika kundi la Ufugaji Samaki katika Maonesho ya Ndani ya Uwanja Kanda ya Kati na kutunukiwa tuzo maalum (trophy) iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa T...

Timu ya Kikapu yajinoa kualekea SHIMISEMITA Mbeya, 2026

Image
  TIMU ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ya Mchezo Kikapu itakayoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) inaendelea na mazoezi ya utimamu wa mwili katika uwanja wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dodoma.  

Prof. Nagu awataka wananchi kuzingatia Lishe bora kukuza Uchumi

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   WANANCHI wametakiwa kuzingatia ulaji bora wa chakula kwa ajili ya kuboresha na kulinda afya kwa kutumia mazao yanayozalishwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ili wawe na lishe bora itakayowasaidia kutekeleza majukumu ya kujenga taifa. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya Afya, Prof. Tumaini Nagu alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma. Prof. Nagu aliwasisitiza wananchi kuzingatia ulaji wa chakula bora kwa ajili ya afya bora, akisema kuwa mazao yanayozalishwa katika Jiji la Dodoma ni bora na yanamchango mkubwa katika kuboresha lishe. “Niwapongeze Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri mnayoifanya. Pia niwasisitize wananchi hasa vijana kula chakula bora kama tulivyojionea hapa. Mazao yanayozalishwa ni mazao bora kabisa kwa afya. Hivyo, vijana kama kizazi cha baadae wajitahidi kula ...

Baraza Maalumu la Madiwani Jiji la Dodoma Mrejesho wa Bajeti 2026/2027

Image
 

Taarifa kwa Umma Maingizo ya Shilingi 4,4390,481,496 kutekeleza Miradi ya Maendeleo Dodoma

Image
 

Jiji la Dodoma kuwa kinara ushirikiano na TBS

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewataka maafisa afya na watumishi wa sekta mbalimbali kuimarisha ushirikiano na kutumia ipasavyo mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuongeza ufanisi katika ukaguzi na usajili wa bidhaa. Akifungua mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Sebastian Pima alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo washiriki kutumia mfumo wa TBS kwa usahihi ili shughuli zote za ukaguzi na usajili ziweze kufanyika kwa ufanisi kupitia mfumo huo. “Kila mmoja anatakiwa kushirikiana na wenzake, hizi ni kazi za timu, si za mtu mmoja. Tunataka Dodoma iwe mfano wa kuigwa nchini katika utekelezaji wa majukumu ya ushirikiano kati ya TBS na halmashauri, kila afisa atapangiwa malengo ya kila siku na kila wiki yatakayosaidia kuongeza utendaji na kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kuboresha huduma kwa wananchi," alisema Dkt. Pima. Aidha, aliwahimiza washiriki kutumia fursa ya uwepo wa...

Dodoma Jiji yajiandaa Ngoma na Kwaya SHIMISEMITA, 2026

Image
    Watumishi wa Timu ya Halmasahuri ya Jiji la Dodoma inayoshiriki Mashindano ya SHIMISEMITA 2026 jijini Mbeya wanaendelea na kujifua katika mazoezi makali kwa ajili ya mashindano ya ngoma na kwaya, mazoezi yanayoendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma. Mashindano ya SHIMISEMITA ya Mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tupo Tayari kwa AFCON 2027”.  

Teknolojia ya Kinengunengu mkombozi kwa vifaranga vya kuku Dodoma

Image
  Na. Mwandishi wetu, NZUGUNI Halmashauri ya Jiji la Dodoma limeibua ubunifu mpya wa teknolojia ya banda maalumu la kufugia vifaranga vya kuku maarufu kama ‘Kinengunengu’ linalolenga kuwasaidia wafugaji kupata njia bora ya kuwapatia vifaranga joto, chakula, malazi na mazingira salama ya ukuaji. Banda hilo limekuwa miongoni mwa vivutio vikubwa katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni kupitia banda la Jiji la Dodoma, ambapo wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kujifunza namna ya kuanza na kuendeleza ufugaji wa kuku kwa njia rahisi na salama. Akielezea banda hilo, Afisa Mifugo wa Jiji la Dodoma, Delila Mlamka alisema kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakitegemea matumizi ya taa na mkaa kwa ajili ya kuwapatia vifaranga joto, lakini teknolojia ya Kinengunengu imekuja kuondoa utegemezi huo kwa kutumia muundo unaoweza kuhifadhi joto ndani ya banda. Alisema kuwa Kinengunengu kimeundwa katika mfumo wenye sehemu mbili muhimu, sehemu ya kul...

Silage suluhisho la uhaba wa chakula cha ng'ombe Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, NZUGUNI Wafugaji wa ng’ombe katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehimizwa kuanza kutengeneza na kuhifadhi chakula cha mifugo kilichochachushwa (Silage) ili kuhakikisha mifugo inapata lishe ya kutosha wakati wa kiangazi, kipindi ambacho maeneo mengi hukumbwa na upungufu mkubwa wa malisho kutokana na ukame. Rai hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Delila Mlamka wakati akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la mifugo la halmashauri hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini hapa. Alisema kuwa Silage ni chakula kinachotengenezwa kwa kuchanganya majani mabichi yaliyokatwakatwa, kiasi kidogo cha majani makavu, pumba na molases, kisha kuhifadhiwa kwenye mazingira yasiyoruhusu hewa ya oksijeni kuingia kwa siku 21 ili kichachuke vizuri na kuwa salama kwa matumizi ya mifugo. Alisema kuwa chakula hicho   kinaweza kutengenezwa kwenye mashimo au mapipa na kuhifadhiwa katika mifuko midogo ya plastiki na mifuko maalumu ya k...