Bucha 59 za uuzaji nyama Kanda Namba Sita zakaguliwa

Na. Mwandishi Wetu, MIYUJI

Timu ya wataalamu kutoka Kanda Namba Sita imefanya operesheni maalum ya kukagua bucha za nyama na samaki, lengo likiwa ni kudhibiti uuzaji wa nyama ambayo haijakaguliwa wala kupigwa muhuri na mamlaka husika ili kulinda afya za walaji.




Akizungumza wakati wa kuhitimisha zoezi lililofanyika takribani kwa siku tatu, Afisa Mifugo Kanda Namba Sita, Prisca Henry alisema kuwa jumla ya bucha 59 zimekaguliwa ambapo ukaguzi uliofanyika ulihusisha leseni, usafi wa bucha na vifaa vya kuhifadhia nyama na samaki na uvaaji wa sare kwa wauzaji.

“Zoezi hili limetufanya kujua jumla ya idadi ya bucha zilizopo kwenye kanda hii, pia imetupa fursa ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara mmoja mmoja kuhusu usafi na umuhimu wa kulipa leseni, ushuru wa huduma na upimaji wa afya kwa wauzaji” alisema Henry.

Alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kila mwezi watafanya ukaguzi ili kutokomeza uuzaji haramu wa nyama na mazao yatokanayo na mifugo na samaki.







MWISHO

Comments

Popular Posts

Msalato wamshukuru Rais, Dkt. Samia ujenzi wa shule

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni nyenzo ya utendaji kazi serikalini – Dkt. Biteko

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma atembelea Kijiji cha Mitambo, Nanenane