Diwani Kerenge atoa shukrani kwa wananchi kumchagua
Na. Mwandhishi wetu, MNADANI
Diwani wa Kata ya Mnadani, Mugendi Kerenge awashukuru
wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua na kuonesha imani katika uongozi wake,
akisisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kuboresha maisha ya wananchi wa Mtaa wa
Mnadani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Mtaa wa Mnadani alisema kuwa moja ya majukumu yake makuu ni kusikiliza
kero za wananchi, kuzitatua kwa haraka kadri inavyowezekana na kuhakikisha
maendeleo yanashikamana na mahitaji halisi ya wananchi.
“Najivunia kuwa kiongozi wenu, lakini nawaomba
tushirikiane kwa moyo mmoja, kila kero yenu ni muhimu kwangu, na tutaendelea
kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha matatizo yanapatiwa ufumbuzi” alisema
Kerenge.
Aidha, alisisitiza kuwa mikutano kama hiyo ni nafasi
muhimu ya wananchi kutoa maoni, mapendekezo na kushirikiana na uongozi wa kata
ili kuhakikisha huduma zinaboreshwa, zinapatikana kwa wakati na zinakidhi
mahitaji ya wananchi wote.
Diwani Kerenge aliahidi kuendelea kufuatilia na kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi, huku akisisitiza kuwa maendeleo ya kata ya
Mnadani yanahitaji ushirikiano kati ya viongozi na wananchi.
Comments
Post a Comment