Posts

TAKUKURU yapewa rai kuboresha mikakati ya kutokomeza rushwa

Image
Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeeleza kuwa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania imejipanga kutoa elimu na kusisitiza wananchi kuepuka kupokea rushwa kwaajili ya kuchagua viongozi. Hayo yalielezwa na Mratibu wa Banda la TAKUKURU, Suzana Raymond wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma aliyetembelea banda hilo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa banda la TAKUKURU limejikita katika kutoa elimu na kupokea taarifa zinazohusu masuala ya rushwa. “ Pamoja na majukumu yote, wakati mwingine tunapokea ushauri mbalimbali kwasababu sisi tunaweza tusione tunachokifanya lakini walio nje ndio wanaona nini tunakifanya na huwa tunapeleka ngazi za juu na wao wanazifanyia kazi kwa kadri inavyotakikana ” alisema Raymond . Alisema k u wa lengo la kuwepo katika maonesho ya Nanenane ni kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa jamii hasa kuelekea uchaguzi mkuu. “Lakini katika...

DC Shekimweri ashauri TMDA kuwa wabunifu

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj. Jabir Shekimweri, ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuwa wabunifu na kutumia teknolojia ya kisasa katika shughuli zake za ukaguzi wa dawa na vifaa tiba nchini, ili kuongeza ufanisi na kuimarisha usalama wa wananchi. Alisema hayo wakati alipotembelea banda la TMDA katika Maonesho ya Wakulima Nane n ane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma. Alisema kuwa an a wapongeza kwa kuendelea kutoa huduma ikiwemo kusajili, kudhibiti na kufuatilia ubora wa dawa . “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kulinda afya za wananchi kupitia udhibiti wa dawa na vifaa tiba. Hata hivyo, katika dunia ya sasa ya teknolojia, mnapaswa kuwa wabunifu zaidi katika mbinu zenu za ukaguzi ili kuweza kufika maeneo mengi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi na kuendele a kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya dawa” alisema Alhaj. Shekimweri. P ia aliongezea kwa kuwasisitiz a kuendelea kushirikiana kwa karibu na vyombo ...

Teknolojia Bunifu ya Mifugo yasogezwa maonesho ya Nanenane

Image
Na. Husna Rajabu, DODOMA Taasisi ya Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) imeteka umakini wa wageni katika maonesho ya Nanenane jijini Dodoma kwa kuonesha teknolojia bunifu zinazolenga kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na kuboresha maisha ya wafugaji. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Utafiti na Huduma za Ushauri (LITA), Joseph Msemwa, alisema kuwa taasisi hiyo imeweka bayana bidhaa na huduma kadhaa ambazo ni matokeo ya kazi za vijana wa kitanzania. Alisema kuwa maonesho ya Nanenane ni sehemu muhimu ya kuonesha bidhaa na teknolojia zitakazobadilisha taswira ya uchumi wa wananchi. “Tupo hapa kwenye maonesho ya Nanenane jijini Dodoma, tumeleta teknolojia mbalimbali zinazohusiana na bidhaa za maziwa. Pia tuna teknolojia ya uchakataji wa ngozi ambapo tunawafundisha vijana wetu namna ya kuchakata ngozi, kuanzia ikiwa mbichi mpaka ifike hatua ya mwisho ya utengenezaji wa bidhaa. Kama mnavyojionea bidhaa za ngozi zipo za aina tofauti tofauti ikiwemo viatu, heren...

Sura mpya ya kilimo cha vitunguu yaonesha mafanikio

Image
Na. Husna Rajabu, DODOMA Kitunguu kimekuwa ni miongoni mwa zao la biashara chenye faida kubwa na hulimwa karibu maeneo yote nchini hasa maeneo ya miinuko ya kaskazini mwa Tanzania. Katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma vipando bustani vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma vimejumuisha teknolojia ya ulimaji vitunguu kwa njia ya asili katika eneo dogo na kupata mazao mengi. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Madei Kidai alieleza mchakato wa kilimo hicho chenye tija kibiashara. “Ili kufanikisha kilimo cha vitunguu, ni lazima uanze na maandalizi ya shamba. Pia, tunawahimiza wakulima kutafuta mbegu bora, kuandaa matuta vizuri, na kuhamisha miche kutoka kwenye kitalu baada ya muda muafaka. Hapa kwetu tumetumia mbinu hizi, na matokeo yanaonekana kama hivi mnavyoona” alieleza Kidai. Kwa mujibu wa Kidai, baada ya kupanda, hatua muhimu zinazofuata ni umwagiliaji na udhibiti wa wadudu na magonjwa. Alisisitiza kuwa wametumia v...

Dodoma Jiji FC yatangaza benchi la ufundi msimu wa 2025/2026

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, imemtambulisha Mashami Vicent raia wa Burundi kuwa kocha wake mkuu kuelekea kwenye msimu wa mashindano ya ligi kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/2026, sanjari na hilo imemtambulisha Bakira Guy raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo. Hayo yalibainishwa na Novatus John, Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji FC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Vizano jijini Dodoma ukiwa na lengo la kutambulisha benchi jipya la ufundi. “Baada ya kuvunja benchi letu zima la ufundi tulilokuwa nalo msimu uliopita, kama uongozi tulikaa chini na kuanza mchakato rasmi wa kutafuta benchi jipya la ufundi. Tulikuwa makini kupitia “CV” za makocha mbalimbali hatimae tukaweza kupata kocha bora zaidi ya wote na ndiye huyu ambaye tumemtangaza. Kwa upande wetu tutampatia stahiki zake zote ili timu yetu ifanye vizuri zaidi msimu ujao” alisema John. Mashami Vicent kabla ya kutuwa Dodoma J...

Vipando bustani vya Jiji la Dodoma yamvutia DC, Dkt. Mashinji

Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vi n cent Mashinji ametembelea banda la vipando bustani ya mbogamboga la Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kujionea aina mbalimbali za mboga na matunda zilizoandaliwa kwaajili ya kutolea elimu na kuhamasisha wananchi kuzingatia mlo kamili. Teknolojia hizo za kisasa zinawezesha mbogamboga kupandwa kwenye vitu mbalimbali kama kiroba, kopo la maji au eneo dogo kutokana na ufinyu wa maeneo na zikaendelea kustawi kwa ubora unaotakiwa. Baada ya kupewa maelezo ya kina kuhusiana na aina mbalimbali za teknolojia ya upandaji wa mbogamboga ali sema kuwa anawapongeza wataalam kwa kubuni njia za kisasa za kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema. “ Hiki kilimo cha mjini mnapaswa kukiangalia kwa jicho la ziada kwa kuhakikisha mnatoa elimu nzuri zaidi, lakini pia mshirikiane na watu wa mipango miji ili kuhakikisha watu wanapata maeneo mazuri yenye nafasi ya kufanya hiki mnachowaelekeza ” alisema Dkt. Mashinji. Kwa upande wake Afis...

Dkt. Mashinji: Tuimarishe Ubunifu wa Kilimo cha Zabibu Dodoma

               Na. Leah Mabalwe , DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vi n cent Mashinji amewataka m aafisa k ilimo wa Jiji la Dodoma kuongeza juhudi na ubunifu katika kukuza kilimo cha zabibu, kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wa Jiji la Dodoma. Hayo aliyasema mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho ya kilimo Nanenane , ambapo alipata fursa ya kuona bidhaa mbalimbali zinazotokana na zabibu, ikiwemo juisi, divai na zabibu kavu. A li sema kuwa pamoja na jitihada zinazofanyika, bado kuna nafasi kubwa ya kuboresha na kuongeza thamani katika zao hilo. “ Jiji la Dodoma l ina nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha zabibu Afrika Mashariki. Kwa upande wenu nyie maafisa kilimo mnapaswa kuwa wabunifu zaidi na hata kufuata zile kanuni ambazo zao hili la zabibu linapaswa kuwa hasa katika hatua ya upandaji” alisema Dkt. Mashinji. Kwa upande wake Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Emmanuel Mayyo...

Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi wapewa Semina Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wametakiwa kusoma katiba, sheria na miongozo inayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Msisitizo huo ulitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba, Wakili Cosmas Nsemwa wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alianza kwa kuwapongeza washiriki wa mafunzo kwa kuteuliwa kuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata. “Someni kwa umakini katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na ulizeni maswali ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine pengone yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekelezaji wenu wa kazi za uchaguzi” alisema Wakili Nsemwa. ...

Kilimo cha Mbogamboga kukuza Afya na kipato kwa wananchi Jiji la Dodoma

Na. Eupilio Anthony, DODOMA Mamia ya wananchi wameonesha hamasa kubwa kutembelea mabanda ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma yenye teknolojia mpya za kilimo, mifugo bora, ufugaji wa kisasa wa samaki, pamoja na bidhaa za viwandani zinazotengenezwa na wajasiriamali wa ndani kutokana na mazao ya kilimo na mifugo katika maonesho ya Nanenane. Kauli hii ilitolewa na Afisa Kilimo Mwandamizi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri alipozungumza na waandishi wa habari waliofika kwenye banda la kilimo cha mbogamboga upande wa bustani kwenye maonesho ya wakulima Nanenane Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa kilimo cha kisasa cha mbogamboga kina njia nyingi za kukifanya kiwe na faida kwa afya na kiuchumi. “Hapa tunakipando cha bustani kichuguu ambacho tumepanda mboga mbalimbali, tuna mboga tofauti tofauti ambazo tunazitumia nyumbani. Kwa sasa tunahamasisha wananchi kulima mboga mboga hata kwenye maeneo madogo ya nyumbani kwao, kwa kutumia vichuguu kwasababu ni njia rahisi na safi sana. Pia...

Afisa Biashara Jiji la Dodoma aelezea umuhimu wa kuanzisha Kanda za Huduma

Image
Na. Ramla Makamba, HOMBOLO BWAWANI Katika kuhakikisha huduma za mapato zinapatikana kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanzisha mfumo wa kanda zitakazohudumia wakazi wa kata mbalimbali kwa karibu ambapo wataalamu watakuwa katika maeneo mbalimbali kutoa huduma hizo zikiwemo huduma za ukataji wa leseni ambapo mpango huo utaanza mapema mwezi Agosti, 2025. Wananchi watapata huduma kama vile za ulipaji wa tozo mbalimbali katika maeneo yao bila kulazimika kufuata huduma Katikati ya jiji ikiwa ni miongoni mwa harakati za kutatua changamoto za umbali wa upatikanaji wa huduma pamoja na kuhakikisha ukusanyaji thabiti wa mapato ya serikali ambapo mwanzoni yalikuwa hayafanywi kikamilifu. Hayo yalisemwa na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fikiri Mtoi, katika kikao kilichofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani jengo la utawala, na kuhudhuriwa na watendaji wa kata, watendaji wa mitaa, wenyeviti wa mitaa na wadau wa b...