Posts

Vipando bustani vya Jiji la Dodoma yamvutia DC, Dkt. Mashinji

Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vi n cent Mashinji ametembelea banda la vipando bustani ya mbogamboga la Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kujionea aina mbalimbali za mboga na matunda zilizoandaliwa kwaajili ya kutolea elimu na kuhamasisha wananchi kuzingatia mlo kamili. Teknolojia hizo za kisasa zinawezesha mbogamboga kupandwa kwenye vitu mbalimbali kama kiroba, kopo la maji au eneo dogo kutokana na ufinyu wa maeneo na zikaendelea kustawi kwa ubora unaotakiwa. Baada ya kupewa maelezo ya kina kuhusiana na aina mbalimbali za teknolojia ya upandaji wa mbogamboga ali sema kuwa anawapongeza wataalam kwa kubuni njia za kisasa za kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema. “ Hiki kilimo cha mjini mnapaswa kukiangalia kwa jicho la ziada kwa kuhakikisha mnatoa elimu nzuri zaidi, lakini pia mshirikiane na watu wa mipango miji ili kuhakikisha watu wanapata maeneo mazuri yenye nafasi ya kufanya hiki mnachowaelekeza ” alisema Dkt. Mashinji. Kwa upande wake Afis...

Dkt. Mashinji: Tuimarishe Ubunifu wa Kilimo cha Zabibu Dodoma

               Na. Leah Mabalwe , DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt. Vi n cent Mashinji amewataka m aafisa k ilimo wa Jiji la Dodoma kuongeza juhudi na ubunifu katika kukuza kilimo cha zabibu, kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wa Jiji la Dodoma. Hayo aliyasema mara baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho ya kilimo Nanenane , ambapo alipata fursa ya kuona bidhaa mbalimbali zinazotokana na zabibu, ikiwemo juisi, divai na zabibu kavu. A li sema kuwa pamoja na jitihada zinazofanyika, bado kuna nafasi kubwa ya kuboresha na kuongeza thamani katika zao hilo. “ Jiji la Dodoma l ina nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha zabibu Afrika Mashariki. Kwa upande wenu nyie maafisa kilimo mnapaswa kuwa wabunifu zaidi na hata kufuata zile kanuni ambazo zao hili la zabibu linapaswa kuwa hasa katika hatua ya upandaji” alisema Dkt. Mashinji. Kwa upande wake Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Emmanuel Mayyo...

Wasimamizi Wasaidizi Uchaguzi wapewa Semina Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wametakiwa kusoma katiba, sheria na miongozo inayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Msisitizo huo ulitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba, Wakili Cosmas Nsemwa wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alianza kwa kuwapongeza washiriki wa mafunzo kwa kuteuliwa kuwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata. “Someni kwa umakini katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na ulizeni maswali ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine pengone yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekelezaji wenu wa kazi za uchaguzi” alisema Wakili Nsemwa. ...

Kilimo cha Mbogamboga kukuza Afya na kipato kwa wananchi Jiji la Dodoma

Na. Eupilio Anthony, DODOMA Mamia ya wananchi wameonesha hamasa kubwa kutembelea mabanda ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma yenye teknolojia mpya za kilimo, mifugo bora, ufugaji wa kisasa wa samaki, pamoja na bidhaa za viwandani zinazotengenezwa na wajasiriamali wa ndani kutokana na mazao ya kilimo na mifugo katika maonesho ya Nanenane. Kauli hii ilitolewa na Afisa Kilimo Mwandamizi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri alipozungumza na waandishi wa habari waliofika kwenye banda la kilimo cha mbogamboga upande wa bustani kwenye maonesho ya wakulima Nanenane Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa kilimo cha kisasa cha mbogamboga kina njia nyingi za kukifanya kiwe na faida kwa afya na kiuchumi. “Hapa tunakipando cha bustani kichuguu ambacho tumepanda mboga mbalimbali, tuna mboga tofauti tofauti ambazo tunazitumia nyumbani. Kwa sasa tunahamasisha wananchi kulima mboga mboga hata kwenye maeneo madogo ya nyumbani kwao, kwa kutumia vichuguu kwasababu ni njia rahisi na safi sana. Pia...

Afisa Biashara Jiji la Dodoma aelezea umuhimu wa kuanzisha Kanda za Huduma

Image
Na. Ramla Makamba, HOMBOLO BWAWANI Katika kuhakikisha huduma za mapato zinapatikana kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanzisha mfumo wa kanda zitakazohudumia wakazi wa kata mbalimbali kwa karibu ambapo wataalamu watakuwa katika maeneo mbalimbali kutoa huduma hizo zikiwemo huduma za ukataji wa leseni ambapo mpango huo utaanza mapema mwezi Agosti, 2025. Wananchi watapata huduma kama vile za ulipaji wa tozo mbalimbali katika maeneo yao bila kulazimika kufuata huduma Katikati ya jiji ikiwa ni miongoni mwa harakati za kutatua changamoto za umbali wa upatikanaji wa huduma pamoja na kuhakikisha ukusanyaji thabiti wa mapato ya serikali ambapo mwanzoni yalikuwa hayafanywi kikamilifu. Hayo yalisemwa na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fikiri Mtoi, katika kikao kilichofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani jengo la utawala, na kuhudhuriwa na watendaji wa kata, watendaji wa mitaa, wenyeviti wa mitaa na wadau wa b...

Wenyeviti Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani wapewa mafunzo huduma ndogo za kifedha

Image
Na. Rehema Kiyumbi, HOMBOLO BWAWANI Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma latoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Hombolo Bwawani juu ya matumizi ya fedha na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kiuchumi. Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Abdallah alisema kuwa elimu ya huduma za kifedha ni muhimu kwa wananchi ili kuweza kufahamu namna ya kufanya matumizi na kuweka akiba. Alisema kuwa kikao hicho kimewahusisha wenyeviti wa serikali za mitaa kwasababu ndio viongozi wa karibu na wananchi. “Hii elimu ya huduma za fedha, tunayowaletea ni mahsusi kwenu kwasababu itawasaidia kufanya maamuzi sahihi wakati wa matumizi. Lakini pia, katika kutunza na kuweka akiba. Huduma ndogo za mikopo ya fedha, mikopo ya vitu na vifaa mbalimbali, mikopo ya nyumba, elimu ya ujasiriamali pamoja na huduma za bima ya afya na bima ya mali ni muhimu kufahamu ili kuwa katika mazingira salama ya ku...

Jiji la Dodoma lapewa angalizo lishe bora kwa wananchi

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Katibu Tawala Mkoa wa Singida, ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuelezwa shughuli zinazotolewa katika banda hilo kwa upande wa Divisheni ya Kilimo Mjini. Alielezwa kuwa Kilimo Mjini kinahusiana na kilimo cha kisasa kinachojikita katika mbogamboga na matunda kutokana na ufinyu wa maeneo ya mjini wanapoishi wakulima. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Athumani Mpanda alieleza kuwa wakulima wanapaswa kutumia maeneo yao madogo waliyonayo kwaajili ya bustani kiroba. “Hizi bustani kiroba tunazitumia kupanda mbogamboga ambazo familia itatumia na hii ni kwasababu kama una kiroba cha kustawisha maua ambayo huyatumii ni vizuri kutumia kuotesha mboga mboga ambazo zitajumuisha lishe na kupendezesha mazingira yetu” alisema Mpanda. Aliongeza kuwa elimu ya bustani za majumbani imeendelea kutolewa katika taasisi nyingi za serikali pamoja na shule za msingi na sekondari. “Tumeanzisha elimu hii kwa lengo la kuhakikisha wakulima na wale ...

TARURA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE NZUGUNI JIJINI DODOMA

Image
#Yajipanga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu ushiriki wa vikundi vya kijamii katika matengenezo ya barabara nchini   Na. Mwandishi Wetu, DODOMA  Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.  TARURA inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA, Catherine Sungura amesema kuwa TARURA imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia yanayohusu ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini. Kwa mujibu wa Sungura baadhi ya maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii. "Kupitia wataalamu wetu ambao wapo katika banda letu tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau wetu wengine namna wanavyoweza kus...

Fursa ya Ufugaji wa Mbwa katika Jiji la Dodoma

Image
                                                                 Na Eupilio Anthony, DODOMA Maonesho ya sherehe za wakulima nchini inazofahamika kama Nanenane, wananchi wajitokeza kujionea mifugo, bidhaa za kilimo, uvuvi na bidhaa zilizosindikwa na wajasiliamali kutokana na mazao hayo huku wakifurahishwa na ufugaji wa mbwa kisasa. Moja kati ya wafugaji na mfanyabiashara wa mbwa, Mwakaleli Mwakasege aliwaeleza wananchi anavyofanya biashara hiyo. “Mimi ni mfugaji wa mbwa kwa zaidi ya miaka 10 na leo kwenye sherehe hizi za Nanenane nimefurahi sana kuona jamii inaanza kutambua thamani ya mnyama huyu. Mbwa si tu mnyama wa kufuga kwa ajili ya ulinzi ni rafiki mkubwa wa familia, mlinzi wa mali, na kwa sasa, chanzo cha kipato kwa watu wengi kama mimi” alisema Mwakasege. Aliendelea kueleza tabia za mbwa anapoishi na binadamu ku...

RC Dendego apeleka salamu za Waziri Bashe Nanenane

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego aeleza kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza vipaumbele vya kilimo ili kuongeza tija za uzalishaji, kuchangia ongezeko la ajira pamoja na ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta ya kilimo. Aliyasema hayo wakati akisoma salamu za Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa ufunguzi wa maonesho Nanenane ya wakulima, wafugaji na wavuvi uliofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma kuanzia tarehe 01 – 08 Agosti, 2025. Alisema kuwa zipo hatua zitakazosimamiwa na wizara katika kuhakikisha nchi inakua na chakula cha kutosha wakati wote. “Wizara inatazamia kuimarisha upatikanaji wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi. Pia kuimarisha maendeleo ya ushirika na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa sekta ya kilimo” alisema Dendego. Alimalizia kwa kusema kuwa wizara imeendelea kuwashauri, kuwael...