Posts

Shilingi Milioni 473 kutekeleza Mradi wa Ufungaji CCTV Kamera Jiji la Dodoma

Image
Na. Josephina Kayugwa, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesani mkataba na Kampuni ya Wisjane Smart Systems kwaajili ya ufungaji wa kamera za usalama barabarani (CCTV) unaogharimu shilingi 473,000,000 ikiwa ni mradi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu. Akitoa taarifa ya mradi, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa mradi huo utakwenda kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dodoma kwasababu kamera hizo zitafanya kazi masaa 24. “Mradi huu wa gharama ya shilingi 473,000,000 utahusisha ufungaji wa kamera kwenye barabara zinazoinga njia kuu lakini pia hapo baadae utakuja kuimarishwa zaidi kwa kuongeza sehemu nyingine za kuweka kamera lengo ni kupata picha zote za vyombo vya usafiri vitakavyokuwa vikiingia na kutoka katika Jiji la Dodoma” alisema Fungo. Aliongeza kuwa wana mpango wa kuunganisha mfumo huo na taasisi nyingine ili kuimarisha ulinzi na usalama. “Mfumo huu baada ya muda tuta...

Shule ya Sekondari ya Bil. 3.9 kujengwa Kata ya Chahwa

Image
Na. Emanuel Charles, CHAHWA Hafla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Chahwa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 baina ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkandarasi kutoka Gopa contractors Tanzanian Limited imefanyika katika Kata ya Chahwa ukilenga kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi. Mradi huo unatekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukiwa ni ujenzi wa shule ya ghorofa nne yenye madarasa 12, maktaba pamoja na maabara nne, chumba cha TEHAMA na jengo la utawala na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja. Akizungumza katika utiaji saini wa ujenzi wa shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuleta miradi mikubwa katika maeneo ya nje ya Mji wa Dodoma. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa mradi huu mkubwa kwasababu unaenda kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, ndugu zangu ni wakati sasa maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma yanufaike...

Soko la Sabasaba kuongozwa kwa misingi ya uongozi bora

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Kaimu Mkuu Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abdul Chacha amewaasa viongozi wa Soko la Sabasaba kuzingatia weledi katika kufanya kazi zao ili kuiishi dhana ya uongozi bora. Aliyasema hayo katika mafunzo waliyoandaa kwa viongozi wa Soko la Sabasaba yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo kikuu cha Mabasi Dodoma. Alisema kuwa sifa mojawapo kubwa ya kiongozi bora ni yule mwenye kuzingatia katiba au muongozo wa ushirika ili aweze kutenda haki. “Kiongozi bora ni yule anayejua namna ya kutuimia katiba vizuri. Labda niulize hapa, Katiba ya ushirika ipo? Kama ipo, je ilitumika wakati ule matatizo yameanza kutokea? Jibu litakua hapana. Nipende kuwaambia kuwa, ukiijua vizuri katiba na miongozo, ni rahisi sana Kutenda haki kwasababu utatenda haki kwa kuzingatia taratibu na hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa” alisema Chacha. Aliongeza kuwa zipo sifa zaidi ya 25 za kiongozi bora ambapo kila kiongozi wa soko la sabasaba anapaswa ...

Bima ya Taifa ya Afya yatoa huduma kieletroniki

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA Maboresho ya huduma ya Bima ya Afya yamefanywa kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia ambapo wananchi wanaweza kujisajili kupata huduma za bima kupitia simu zao na vifaa vya kieletroniki vyenye ‘Internet’. Hayo yalisemwa na Afisa Wanachama Mwandamizi, Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma, Bakary Hamdun katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri wakati akiwasilisha sheria ya afya na kanuni zake. Alisema kuwa kila mwanachama anaetarajia kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) anaweza kujihudumia kupitia simu ya mkononi “Mwanachama yeyote awe mtumishi au mwananchi wa kawaida anaweza kujisajili kupitia simu yake ya mkononi. Na anaweza kufanya hivyo bila kuwa na changamoto ya aina yoyote kwasababu huduma hii ni rahisi pia inafanyika kwa muda mfupi” alisema Hamdun. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe aliipongeza serikali kwa hatua kubwa ya uboresha...

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ahimiza matumizi ya mfumo NeST

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko aeleza kuwa mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma NeST katika kufanya manunuzi ya vifaa vya serikali ni mfumo rafiki unaorahisisha manunuzi na kuweka taarifa hizo katika hali ya usalama. Aliyazungumza hayo katika Baraza la Madiwani la kawaida liliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa madiwani. Alisema kuwa mfumo wa manunuzi wa NeST upo tayari kwa mujibu wa sheria na umeonyesha matokeo chanya. “Niwajulishe ndugu wajumbe ya kwamba, mfumo huu hatuna namna ya kuepuka kuutumia kwasababu ndio mfumo ambao tunapaswa kuwa nao ili kufanikisha manunuzi ya vifaa mbalimbali vya serikali” alisema Dkt. Sagamiko. Aliongeza kuwa mfumo haumlazimishi mnunuzi kununua kila kitu kwa wakati mmoja. “Mfumo huu unahitaji ushirikiano ili uweze kufanya manunuzi yako. Kikubwa ni wewe kuhakikisha unafahamu unafanya manunuzi ya kiwango gani. Hakikisha unafahamu...

Shule mpya ya Msingi Chinyoyo ya kwanza kujengwa Kata ya Kilimani

Image
Na. Emmanuel Charles, KILIMANI Mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Chinyoyo, Kata ya Kilimani unaogharimu shilingi 147,000,000 ni shule ya kwanza kujengwa katani hapo na itaondoa adha ya wanafunzi ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo. Haya yalisemwa na Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘Media Tour’ kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia 2021-2025 katika kata hiyo. Alisema kuwa kwasababu kata yake ipo mjini, miundombinu ikiwemo ya elimu ilichelewa kufika na sasa serikali ya awamu ya sita inajenga shule ya msingi ili kuwakwamua watoto wanaotembea umbali mrefu. “Kwa miaka yote ya nyuma, kata hii haikuwahi kuwa na shule yeyote na wanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata masomo katika kata za jirani. Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuona na kuamua kutenga eneo la kujenga Shule ya Msingi Chinyoyo kwa gharama ya shilingi 147,000,000 ambapo ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili...

Kata ya Kilimani mbioni kujenga Ofisi kila Mtaa

Image
Na. Emmanuel Charles, KILIMANI Kata ya Kilimani yatenga kiasi cha shilingi 150,000,000 kwaajili ya ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa katika mwaka wa fedha 2025/2026 lengo ikiwa ni kusogeza huduma karibu kwa wananchi. Haya yalisemwa na Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko alipokua akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ‘Media Tour’ kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kuanzia mwaka 2021-2025. Diwani Mwaluko alisema kuwa Kata ya kilimani ina maeneo ya kutosha kwaajili ya kujenga ofisi za mitaa na wapo wananchi wametoa maeneo yao zijengwe ofisi za mitaa. “Katika yetu tumeazimia kujenga ofisi kwa kila mtaa, lengo letu ni kusogeza huduma kwa jamii. Kuna baadhi ya huduma mwananchi sio lazima aende ofisi ya kata kumfuata afisa mtendaji wa mtaa, ofisi ya mtaa ikiwepo ni rahisi na hatapoteza muda kupata huduma yake. Yupo pia mwananchi mwenye mapenzi mema na maendeleo ya kata, amejitolea eneo lake ijengwe ofisi, tunamshukuru sana” alisema Diwani Mwaluko. Al...

Uwanja wa Michezo Kilimani utumike kuboresha Afya za wananchi

Image
Na. Nancy Kivuyo, KILIMANI Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko amesema suala la michezo katika kata yake linapewa kipaumbele kupitia hamasa ya ugawaji wa jezi na mipira pamoja na kuhimiza wananchi kupenda michezo ili kulinda afya zao. Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kata ya Kilimani kuona shughuli za michezo zinavyofanyika. “Sisi Kata ya Kilimani tunahamasisha sana vijana wetu na watu mbalimbali kushiriki michezo kwasababu tunatambua michezo ni ajira lakini pia michezo ni afya. Bonanza na michezo mingi imekuwa ikifanyika katika uwanja wetu hali inayoonesha ni namna gani kata yetu ni kielelezo bora katika kuhamasisha michezo” alisema Diwani Mwaluko. Aliongeza kuwa vijana wa katani hapo wamekuwa wakipewa jezi na mipira ili kuongeza hamasa ya kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali. “Jambo hili nimeweza kulisimamia kwa vitendo, kunapokuwa na changamoto ya vifaa nimekuwa nikiwapatia jezi pamoja na mipira ili waendeleze vipaji vyao...

Utunzaji Mazingira Kata ya Kilimani kielelezo bora cha kuigwa

Image
Na. Nancy Kivuyo, KILIMANI Kata ya Kilimani yaendelea kuhimiza kwa vitendo utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti mbalimbali ikiwemo ya kivuli pamoja na matunda ili kuweka mazingira safi na ya kuvutia jambo linalowafanya wananchi wake kufurahia mandhari na kuwa na lishe bora. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo kujionea utunzaji wa mazingira unavyofanyika Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko alisema kuwa wanajitahidi kupanda miti ili kuweka mazingira katika hali nzuri inayovutia. “Sisi hapa Kilimani tuna program za kupanda miti kila mwaka. Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kila mwaka inatupatia miche ya miti kwaajili ya kupanda katika kata yetu” alisema Diwani Mwaluko. Aliongeza kuwa wanatoa elimu ya utunzaji mazingira kwa wananchi wa kata hiyo ili kuhakikisha wanakuwa vinara na mfano wa kuigwa katika Jiji la Dodoma. “Kwa ujumla kata yetu inafanya vema katika utunzaji wa mazingira. Kama mnavyojionea sehemu kubwa ni kijani, kila kaya un...

Bonanza la Michezo lahamasisha Wananchi kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jiji la Dodoma

Image
Na. Nancy Kivuyo, UHURU Halmashauri ya Jiji la Dodoma yafanya bonanza la michezo la hamasa kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura awamu ya pili kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha ili wapate haki ya kupiga kura ifikapo mwezi Oktoba, 2025. Hayo yalisemwa na Afisa Mwandikishaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro kabla ya ufunguzi wa bonanza la hamasa kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika uwanja wa michezo wa Mtekelezo katika Kata ya Uhuru, jijini Dodoma. Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura. “Tunategemea kufanya maboresho ya uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili watu wapate sifa ya kupiga kura hapo mwezi Oktoba, 2025. Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina vituo 105 na uandikishaji unategemewa kuanza mnamo tarehe 16 – 22 Mei, 2025” alisema Kimaro. Aliongeza kuwa vituo vitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi n...