Posts

Vyama vya siasa vyapongezwa kudumisha Demokrasia jijini Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Vyama vya siasa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma vimepongezwa kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kuanzia mchakato wa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mpaka hatua ya kampeni za uchaguzi kwa wagombea mbalimbali. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ofisini kwake Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ofisini kwake. Dkt. Sagamiko alivipongeza vyama vya siasa kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika michakato yote ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kuchukua na kurejesha fomu za kugombea uongozi, pingamizi kuhusu uteuzi mpaka zoezi linaloendelea la kampeni za uchaguzi....

Vyama yatakiwa kufanya kampeni za kistaarabu Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA VIONGOZI wa vyama vya siasa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kufanya kampeni za kistaarabu ili Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanyika kwa amani na utulivu. Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko kiongea na waandishi wa habari na wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ofisini kwake leo wakati akiwaelezea mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Dkt. Sagamiko alisema kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Kalenda ya Uchaguzi zinafanyika siku saba kabla ya tarehe ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hivyo, kampeni zilianza jana tarehe 20 Novemba, 2024 baada ya vyama vya siasa kuwasilisha ratiba ya mikutano ya kampeni kwa Msimamizi wa Uchaguzi. Ratiba hizo zilishawasilishwa kwa Mkuu wa Polisi Wila...

Rushwa Adui wa Haki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Muelimishaji wa Darasa Tembezi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Chacha Marwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024 katika vituo husika.   Marwa alitoa elimu hiyo kwa wananchi waliopanda gari tembezi kutoka Soko la wazi la Machinga hadi Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuwakumbusha kuwa haki ya kiongozi bora ipo mikononi mwao.   Alisisitiza kuwa kupiga kura ni msingi wa maendeleo katika mitaa yao kwa kuzingatia haki na kutokupokea rushwa ya aina yoyote kutoka kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti na wajumbe watano (5) wa serikali za mitaa.   “Elimu hii ni muhimu kwa wananchi wote hasa mliojiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapiga kura, ni muhimu sana kupata haki yako ya msingi, msipoenda kupiga kura mtashindwa kupata viongozi bora wa kuleta maendeleo. Mjitahidi kuchagua viongozi wazalendo wenye busara kwa kusikiliza sera zao. Pia walemavu ambao hawezi kufika katika vituo vya kupiga kura, s...

Kura Yako Maendeleo ya Mtaa

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA Timu hamasa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, imeendelea na zoezi la kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.   Zoezi hilo lilifanyika katika eneo la Soko la wazi la Machinga hadi Ihumwa kwa lengo la kuwakumbusha na kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kupiga kura kwasababu ni msingi mzuri wa kuleta maendeleo katika mitaa yao.   Muelimishaji wa katika gari maalum lijulikanalo kama darasa tembezi, Isabella Bruno alisema kuwa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, wametoa gari la darasa tembezi kwa lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.   Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuchagua viongozi wenye sifa kwa kusikiliza sera zao kipindi ambacho kampeni zitakapoanza tarehe 20 Novemba, 2024 na kuangalia kiongozi wa kuwaongoza kwa muda wa miaka mitano ya uongozi. ...

Jiji la Dodoma lasaini mkataba ujenzi wa barabara ya lami kwenda Hospitali ya Jiji

Image
Na. John Malima, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesaini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa barabara kutoka Hospitali ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma hadi barabara kuu ya Singida yenye urefu wa Kilomita 1.6 kwa kiwango cha lami. Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe (kustoto) na Mkurugenzi wa Jiji, Dkt. Frederick Sagamiko wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Mkataba huo ulisainiwa tarehe 20 Novemba, 2024 katika Ofisi ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma baina ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Kampuni ya ujenzi ya Kings Builders Limited ukiwa na thamani ya shilingi 2,431,050,561.63 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Nne Thelathini na Moja Laki Tano na Mia Tatu Sitini na Moja na senti Sitini na Tatu). Katika zoezi la kusaini mkataba huo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alimshukuru Mkandarasi kwa kuunga juhudi za serikali na alimtaka kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa. “Kwanza nawaponge...

Mtaa wa Chikole washauriwa kujitokeza kupiga kura

Image
Na. Faraja Mbise, MSALATO Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wametakiwa kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi walio bora na wenye tija kwa maendeleo ya mitaa yao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Hayo, yalisemwa na mkazi wa Mtaa wa Chikole, Glory Kondo, Kata ya Msalato, alipokuwa akifanyiwa mahojiano kuhusu muitikio wa wananchi kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. “Kuna umuhimu wa kuchagua kiongozi kwasababu ni bora ukamchagua kiongozi ambae unaona kwako wewe atakufaa kuongoza vizuri, kuliko kutokupiga kura ina maana kwamba, utakuwa umeburuzwa, unaweza ukachaguliwa kiongozi ambaye ulikuwa haumuhitaji lakini itabidi ukubaliane nae kwasababu haujajiandikisha ili kuchagua kiongozi unayemtaka. Hivyo, ni muhimu kujiandikisha na ukamchagua kiongozi unayemtaka” alisema Kondo. Akiongolea kuhusu wananchi kujitokeza kupiga kura, alitoa wito kwa wakazi wote waliojiand...

Taasisi zatakiwa kupanda miti kukijanisha Dodoma

Image
  Na. Faraja Mbise, DODOMA Taasisi zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na wananchi, wamehimizwa kupanda miti katika maeneo wanayofanyia kazi na wanayoishi ili kuifanya Dodoma iwe ya kijani na kukabiliana na madiliko ya tabia ya nchi. Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya akipanda mti  Hayo yalisemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Kaspar Mmuya alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali katika zoezi la upandaji miti kwa awamu ya pili lililohusu wazaliwa wa mwezi Novemba lililofanyika tarehe 18 Novemba, 2024 katika eneo la Jakaya Kikwete Square, Chuo Kikuu cha Dodoma. “Tumeshaanza kuyagundua maeneo kama matatu hivi, lakini hili ni la pili tutatekeleza Januari au Februari, tayari tumeshaongea na Halmashauri ya Jiji la Dodoma na watatupatia. Maeneo katika Jiji la Dodoma yapo, Dodoma kuwa kijani inawezekana. Watu wanaishi na historia kuwa Dodoma haistawi, ni kavu, ni kame. Hapana, Dodoma sio kame na mifano ipo, mimi ninawaambieni, tafuteni muda, mzunguke mitaan...

Chama cha AAFP chasifu mchakato wa uteuzi wagombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Faraja Msibe, DODOMA CHAMA cha Alliance for African Farmers (AAFP) kimeridhishwa na mchakato wa uteuzi wa wagombea uliofanywa na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuuita kuwa ulikuwa shirikishi. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa wa Dodoma wa Chama cha AAFP, Fredrick Mapua alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uteuzi wa wagombea, mapingamizi na maamuzi ya rufaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mapua alisema “nimekuja kuzungumzia mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia uteuzi wa wagombea, mapingamizi na maamuzi ya rufaa. Nianze kwa kumshukuru sana Rais, mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya amejaribu sana kusimamia demokrasia nchini. Mchakato ulienda vizuri sana. Tulifanya vikao baina ya wasimamizi wa uchaguzi na vyama vya siasa kwa ajili ya kufanya uchaguzi kuwa huru na wa haki. Hivyo, mchakato ulikuwa shirikishi tangu awali. Kwa chama chan...

Chigongwe watakiwa kujitokeza kupiga kura

Image
Na. Dennis Gondwe, CHIGONGWE WAKAZI wa Kata ya Chigongwe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024 ili waweze kuwachangua viongozi wanaowafaa. Masima Masima (wa pili kushoto) wakati wa kuhamasisha umma  Kauli hiyo ilitolewa na mkazi wa Kata ya Chigongwe, Masima Masima alipokuwa akiwahamasisha wananchi wa kata hiyo kujitokeza siku ya kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alipopata nafasi ya kuhamasisha wakati timu ya uhamasishaji ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofika katani hapo kutoa hamasa kwa wananchi. Masima alisema “mimi binafsi cha kwanza, kupiga kura ni jukumu langu na ni haki yangu ya msingi. Tarehe 27 Novemba, mwaka huu ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunakwenda kumchagua mwenyekiti na wajumbe wake, mimi Masima nipo tayari kushiriki uchaguzi huo”. Kwa upande wa mkazi mwingine wa kata hiyo, Salome Nguji alisema kuwa wanachohitaji wapate kiongozi bor...

Wananchi Chikole wahamasishwa kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, MSALATO Wananchi wa Mtaa wa Chikole wamehamasishwa kujitokeza kushiriki zoezi la kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika maendeleo. Patrick Sebyiga (wa kwanza kushoto) akihamasisha baadhi wa wakazi wa Mtaa wa Chikole Hamasa hiyo ilitolewa na kiongozi wa timu ya hamasa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Patrick Sebyiga alipoongoza timu hiyo kutoa hamasa kwa wananchi wa Mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Sebyiga ambae pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma anaeratibu Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura. “Mtakumbuka tumemaliza zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kazi iliyobaki ni kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024. Mjitokeze kuchagua viongozi wenye sif...