Chama cha AAFP chasifu mchakato wa uteuzi wagombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Na. Faraja Msibe, DODOMA
CHAMA
cha Alliance for African Farmers (AAFP) kimeridhishwa na mchakato wa uteuzi wa wagombea
uliofanywa na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri
ya Jiji la Dodoma na kuuita kuwa ulikuwa shirikishi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa wa Dodoma wa Chama cha AAFP, Fredrick Mapua alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa uteuzi wa wagombea, mapingamizi na maamuzi ya rufaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mapua
alisema “nimekuja kuzungumzia mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia
uteuzi wa wagombea, mapingamizi na maamuzi ya rufaa. Nianze kwa kumshukuru sana
Rais, mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya amejaribu
sana kusimamia demokrasia nchini. Mchakato ulienda vizuri sana. Tulifanya vikao
baina ya wasimamizi wa uchaguzi na vyama vya siasa kwa ajili ya kufanya uchaguzi
kuwa huru na wa haki. Hivyo, mchakato ulikuwa shirikishi tangu awali. Kwa chama
changu tulihudhuria vikao hivyo, nikiwepo mimi binafsi, tulikuwa tulipatiwa
miongozo kila mjumbe nakala yake. Maelezo na kanuzi zilikuwa wazi. Wale wenye
uwezo wa kusoma na kuandika walikuwa wanauwezo wa kusoma nakuelewa nini
kilichokuwa kinahitajika na nini kilichokuwa hakihitajiki katika Uchaguzi wa Serikali
za Mitaa. Maelezo yalikuwa yanajitosheleza kwenye kanuni kama ulizifuata
sidhani kama unaweza kuwa muanga wa wale walioenguliwa katika mchakato wa
uchaguzi huu”.
Alisema
kuwa kufuatia mchakato huo haki ilijaribu kutendeka na ilipatikana. Kwa wale walioona
wameonewa fursa ya rufaa ilikuwepo. “Chama changu tulikaa na kujadili wapi
tunamapungufu na wapi wenzetu wametuzidi ili tusionekane bado wadogo sana. Sisi
tulifuata taratibu na kanuni zote. Hivyo, kwenye chama changu hakuna
aliyeenguliwa kutokana na makosa madogo madogo kama walivyokuwa wakilalamika
vyama tofauti kwenye mitandao ya kijamii. Kwa chama chetu wote tulikuwa makini
na kulifuata maelekezo ya mwongozo” alisema Mapua.
Akiongelea
amani na utulivu alisema kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa. Alisema kuwa chama
chake kimeweka mkakati kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. “Sisi
tunapenda amani, utulivu, siasa safi na salama. Hatupendi kuona watu wakiumia
au kuharibikiwa mali kutokana na siasa. Ukiona mtu anatumia nguvu sana kutaka
madaraka jiulize mara mbili” alisisitiza Mapua.
Katika
hatua nyingine Katibu wa Chama cha Kijamii (CCK) Mkoa wa wa Dodoma, Abuutwahiru
Iddi alisema kuwa mchakato wa kuteua wagombea ulifanyika vizuri ukiwa
shirikishi. “Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa aliitisha vikao mbalimbali
kwa lengo la kufanikisha zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. “CCK nayo
ilishiriki kuhamasisha wananchi wake kuweza kuchukua fomu, zimejazwa na
kurudishwa ofisi za serikali za mitaa kwa mujibu wa kalenda na ratiba. Mchakato
umeenda vizuri na sasa tunajiandaa kufanya kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa
tarehe 27 Novemba, 2024. Chama kinaendelea kuhamasisha wananchi ili kuelewa
zaidi maana ya uchaguzi na waweze kujitokeza kupigia kura viongozi
wanaowahitaji tofauti na kubaki nyumbani na wanapopatikana vongozi ambao
hawawahitaji watabaki kulalamika kwa miaka mitano inayofuata” alisema Iddi.
MWISHO
Comments
Post a Comment