Mtaa wa Chikole washauriwa kujitokeza kupiga kura
Na. Faraja Mbise, MSALATO
Wananchi
wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wametakiwa kutumia haki yao ya msingi na ya
kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi walio bora na wenye tija kwa
maendeleo ya mitaa yao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa
kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Hayo,
yalisemwa na mkazi wa Mtaa wa Chikole, Glory Kondo, Kata ya Msalato, alipokuwa
akifanyiwa mahojiano kuhusu muitikio wa wananchi kujitokeza kupiga kura katika
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Kuna
umuhimu wa kuchagua kiongozi kwasababu ni bora ukamchagua kiongozi ambae unaona
kwako wewe atakufaa kuongoza vizuri, kuliko kutokupiga kura ina maana kwamba,
utakuwa umeburuzwa, unaweza ukachaguliwa kiongozi ambaye ulikuwa haumuhitaji
lakini itabidi ukubaliane nae kwasababu haujajiandikisha ili kuchagua kiongozi
unayemtaka. Hivyo, ni muhimu kujiandikisha na ukamchagua kiongozi unayemtaka”
alisema Kondo.
Akiongolea
kuhusu wananchi kujitokeza kupiga kura, alitoa wito kwa wakazi wote
waliojiandikisha katika orodha ya wapiga kura kujitokeza siku ya kupiga kura na
kuchagua viongozi bora na sio bora viongozi. “Wito wangu kwa waliojiandikisha
ninaomba wajitokeze kuja kupiga kura. Niwajibu wao kupiga kura na kumchagua
kiongozi bora kuliko bora kiongozi na wasikubali kuchaguliwa kiongozi”
alisisitiza Kondo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodaboda, Tawi la Mama lililopo Msalato, Amani Howe,
alizungumzia suala la maendeleo ya mitaa kuwa linajengwa na viongozi walio bora
wenye kujua wajibu wao katika ngazi ya serikali za mitaa.
Kondo
alisema “Ni lazima kuwe na umuhimu wa kuchagua viongozi wa mitaa kwasababu ni
kuangalia maendeleo ya mitaa, endapo kama mwenyekiti aliyepita hajafanya
vizuri, anaweza kuchaguliwa mwingine kwamba anaweza akabadilisha maendeleo ya
mitaa yetu”
Michakato
kadha wa kadha imekwisha kupita katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ikiwemo kujiandikisha
katika orodha ya wapiga kura, uteuzi wa wagombea wa vyama vya siasa na kukata
rufaa kwa wagombea. Sanjari na hayo wananchi watapiga kura kuchagua viongozi
wao wa mitaa na wajumbe wa kamati ya mtaa tarehe 27 Novemba, 2024.
MWISHO
Comments
Post a Comment