Posts

Chigongwe watakiwa kujitokeza kupiga kura

Image
Na. Dennis Gondwe, CHIGONGWE WAKAZI wa Kata ya Chigongwe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024 ili waweze kuwachangua viongozi wanaowafaa. Masima Masima (wa pili kushoto) wakati wa kuhamasisha umma  Kauli hiyo ilitolewa na mkazi wa Kata ya Chigongwe, Masima Masima alipokuwa akiwahamasisha wananchi wa kata hiyo kujitokeza siku ya kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa alipopata nafasi ya kuhamasisha wakati timu ya uhamasishaji ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofika katani hapo kutoa hamasa kwa wananchi. Masima alisema “mimi binafsi cha kwanza, kupiga kura ni jukumu langu na ni haki yangu ya msingi. Tarehe 27 Novemba, mwaka huu ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunakwenda kumchagua mwenyekiti na wajumbe wake, mimi Masima nipo tayari kushiriki uchaguzi huo”. Kwa upande wa mkazi mwingine wa kata hiyo, Salome Nguji alisema kuwa wanachohitaji wapate kiongozi bor...

Wananchi Chikole wahamasishwa kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Image
Na. Dennis Gondwe, MSALATO Wananchi wa Mtaa wa Chikole wamehamasishwa kujitokeza kushiriki zoezi la kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika maendeleo. Patrick Sebyiga (wa kwanza kushoto) akihamasisha baadhi wa wakazi wa Mtaa wa Chikole Hamasa hiyo ilitolewa na kiongozi wa timu ya hamasa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Patrick Sebyiga alipoongoza timu hiyo kutoa hamasa kwa wananchi wa Mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Sebyiga ambae pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma anaeratibu Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura. “Mtakumbuka tumemaliza zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura, kazi iliyobaki ni kujitokeza siku ya kupiga kura tarehe 27 Novemba, 2024. Mjitokeze kuchagua viongozi wenye sif...

Wajasiriamali wanufaika na Nishati Jadidifu Dodoma

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wajasiriamali kutoka kata za pembezoni za Hombolo Makulu, Ipala, Mbalawala, Chihanga na Mnadani katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamenufaika na mradi wa nishati jadidifu kwa matumizi ya uzalishaji uliolenga kuimarisha na kuboresha miradi ya wajasiriamali wa pembezoni. Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Santiel Mmbaga Hayo yalisemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Santiel Mmbaga wakati wa mkutano na wadau mbalimbali wenye lengo mahususi la utoaji taarifa ya utekelezaji wa mradi wa matumizi ya nishaji jadidifu kwa matumizi ya uzalishaji kwa mwaka 2022 hadi 2024 katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma. Mmbaga alisema “halmashauri imeweza kunufaika sana na miradi hii ya Kakute ambayo imetufungia nishati hii jadilifu kwenye maeneo ya pembezoni, kwasababu wananchi wetu walikuwa wanahitaji huduma, walikuwa wanafanya kilimo, walikuwa wanachajisha simu lakini sio kwa kiwango hicho. Lakini saizi k...

Wajasiriamali Jiji la Dodoma wahimizwa kurasimisha biashara zao

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wajasiriamali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehimizwa kurasimisha biashara zao kwa lengo la kuwa na wigo mkubwa wa kuweza kukopa katika taasisi za kifedha kwa sababu watakuwa wanatambulika kwa mujibu wa sheria. Katibu Mtendaji wa Shirika Kakute Projects, Livinus Manyanga akiongea na wadau Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji wa Shirika Kakute Projects, Livinus Manyanga alipokuwa akizungumza na wanufaika wa mradi wa nishati jadidifu, wadau wa serikali, viongozi wa sekta ya biashara na wazalishaji wa teknolojia katika mkutano wa wadau wa mradi wa nishati jadidifu kwa matumizi ya uzalishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa uliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Tumejaribu kufanya kazi kwa karibu sana na vile vikundi ambavyo vimekopeshwa mikopo na halmashauri tofauti na hii misaada ambayo tumeitoa sisi, inaonesha wazi kwamba changamoto namba moja ni kwamba, mjasiriamali mdogo mpaka aweze kurasimisha biashara yake ni hatua ndefu na hawapendi...

Kata ya Mkonze yaanza mafunzo ya 10% kwa vikundi

Image
  Na. Dennis Gondwe, KATA ya Mkonze imeanza kutoa mafunzo kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa bila riba na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwajengea uelewa wa uwepo wa mikopo hiyo na taratibu za kuipata. Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkonze, Theresia Camilius wakati akitoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkonze, Theresia Camilius wakati akitoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Mkonze iliyopo Kata ya Mkonze Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Theresia alisema kuwa mafunzo hayo yanahusisha vikundi vilivyosajiliwa na vinavyotarajia kuomba mkopo, vikundi ambavyo havijasajiliwa na vinatarajia kuomba mkopo ili viweze kufahamu mchakato na kufanya usajili na kuomba mikopo ya asilimia 10. “Matarajio ya mafunzo haya ni walengwa na wanufaika wa mikopo hii waweze kuelewa fedha zina...

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uwazi mtupu Jiji la Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma unafanyika kwa uwazi kwa mujibu wa kanuni zilizopo ili wananchi wafurahie kukua kwa demokrasia. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwenendo na shughuli mbalimbali za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazoendelea ofisini kwake leo. Dkt. Sagamiko alisema kuwa hakuna mpango wowote wenye nia ovu ya kuminya demokrasia kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa. Alisema kuwa tangu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaanza ulikuwa wa wazi na shirikishi ukiruhusu vyama vyote kushiriki kikamilifu. Akiongelea zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za uongozi alisema kuwa vyama vyote 19...

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiwaelezea madiwani kuhusu mafunzo ya kuongeza mapato ya ndani kwa mfumo wa matangazo ya biashara ya kidigitali

Image
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akiwaelezea madiwani kuhusu mafunzo ya kuongeza mapato ya ndani kwa mfumo wa matangazo ya biashara ya kidigitali katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri uliopo Mji wa Serikali Mtumba

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akibadilisha mawazo na aliyekuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Image
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Meya mstaafu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama (kulia) katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri uliopo Mji wa Serikali Mtumba kwenye mafunzo kuhusu kuongeza mapato ya ndani kwa mfumo wa matangazo ya biashara ya kidigitali

Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiwa katika mafunzo ya kuongeza mapato ya ndani kwa mfumo wa matangazo ya biashara ya kidigitali

Image
  Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakiwa wanasikiliza mafunzo ya kuongeza mapato ya ndani kwa mfumo wa matangazo ya biashara ya kidigitali katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri uliopo Mji wa Serikali Mtumba

Mwenyekiti UWT Taifa awataka wanawake kuchangamkia mikopo ya Jiji la Dodoma

Image
  Na. Faraja Mbise. DODOMA Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda amewataka wanawake wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuachana na mikopo ya Kausha damu na mwendokasi inayowanyanyasa na kuwadhalilisha wanawake kutokana na muda wa marejesho na kiwango cha riba kuwa kikubwa na hivyo kushindwa kujikwamua kiuchumi na kuwaongezea umasikini zaidi. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza katika Uzinduzi wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara Masoko yote katika Jiji la Dodoma (UWAWAMA), uliofanyika Cathedral Social Hall, tarehe 01 Novemba, 2024. Chatanda aliwataka wanawake wafanyabiashara kuachana na mikopo ya kausha damu na kujiunga na vikundi ili kupata mikopo ambayo inatolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. "Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluh Hassan imerejesha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na ...