Posts

Mtoto wa kike apewe fursa ya kuongoza

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani, ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 11, jamii imeaswa kumshirikisha mtoto wa kike katika ngazi ya uongozi tangu anapoanza kukua mpaka anapokuwa mtu mzima. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiatives, Rebecca Gyumi alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamaiti, Tarafa ya Mndemu, Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Dodoma katika Tamasha la Msichana Amani Music Festival. “Siku hii katika nchi yetu, tunaongozwa na kaulimbiu ya Msichana na Uongozi, Mshirikishe Wakati ni Sasa. Kupitia jukwaa letu la Agenda ya Msichana, tumeitohoa zaidi kaulimbiu yetu ya kitaifa ambapo tunasema Msichana na uongozi, kwakutumia Fursa za Kidijitali au teknolojia ya kidijitali, kwa maana ya kuangalia namna wasichana wanavyoweza kuonesha uongozi kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye teknolojia ya kidigitali” alisema Gyumi. Wakati akizungumza na kundi la wananchi na watoto wa kike alisema kuwa, ...

Sekunde chache kujiandikisha orodha ya wapiga kura

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Urahisi wa zoezi la kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura umekuwa kivutio kikubwa sana kwa wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024. Wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma waliojitokeza kushiriki zoezi hilo la uandikishaji wameeleza urahisi wake kuwa halichukui muda mrefu. Kwa upande wake Mariamu Paul, mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Mpunguzi aliwashauri wananchi kujitokeza na kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwasababu zoezi halichukui muda mrefu. Aliongeza kuwa ni haki yao ya msingi na inawapa fursa kubwa ya kuchagua viongozi wa serikali ya mtaa wanaowataka na kuwaasa wasisubiri kuchaguliwa na watu wengine. “Nimekuja kujiandikisha na nawashauri wananchi wengine waje. Nimetumia kama sekunde kadaa tu kwa sababu hata haizidi dakika moja kuandikishwa na haichukui hata muda wako” alisisitiza Paul. Peter Agustino, mkazi wa Mtaa wa ...

Mila na Desturi kandamizi mwiba kwa mtoto wa kike

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Tanzania inaungana na mataifa mengine katika kupambana na changamoto ya mila na desturi kandamizi ambazo ni kikwazo kwa mtoto wa kike katika kutimiza ndoto zake hasa katika suala la uongozi. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani yaliyofanywa na Shirika la Msichana Initiaves, jijini Dodoma, Balozi. Liberata Mulamula alisema kuwa am tot desturi kandamizi ni kikwazo kwa binti katika kuzifikia ndoto zake hasa katika uongozi. Balozi Mulamula alisema “mila na desturi kandamizi zinamyima mtoto wa kike haki yake ya msingi ya kwenda shule kusoma. Kwahiyo, zinapunguza idadi ya wanawake kuwa viongozi. Mila na desturi kandamizi ndani ya jamii zinampa mtoto wa kike machaguzi machache ambayo yanapelekea kupoteza watoto wa kike wengi sana”. Aidha, alisisitiza mtoto wa kike kutumia teknolojia kwa lengo la kujifunza na kuelimika hasa katika mitandao ya kijamii. Aliwataka waitumie waitumie kwa ufasaha katika kupata elimu na kuwataka kujitambua n...

Jiji la Dodoma wahamasishwa kujiandikisha orodha ya wapiga kura

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Wananchi wamehamasishwa kujitokeza kwenda kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ifikapo Oktoba 11 hadi 20, 2024 kwa lengo la kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Ushauri huo ulitolewa na Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Kamati ya Mipango miji na Mazingira katika Shule ya Sekondari Umonja iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Karama ambae ni Naibu Meya Mstaafu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alitoa rai kwa wana Dodoma na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kushiriki katika kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura kwa sababu ni muhimu kwa wananchi kutumia haki yao. Alisema kuwa kuwa uchaguzi utawasaidia kupata viongozi bora. “Uchaguzi ni gharama, hivyo serikali hugharamia chaguzi kwa ajili ya kukupa haki wewe mtanzania, ikiwa na maana wanataka uchague kiongozi unayemtaka sio uchaguliwe kiongozi” alise...

Maafisa Waandikishaji Jiji la Dodoma watakiwa kufungua vituo kwa wakati

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Maafisa waandikishaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameaswa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga vituo vya uandikishaji orodha ya wapiga kura unaotarajiwa kufanyika tarehe 11-20 Oktoba, 2024. Wito huo ulitolewa katika mafunzo kwa maafisa waandikishaji wa Jiji la Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi wa Mtumba Complex tarehe 08 Oktoba, 2024 na Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Albert Kasoga. Akizungumza na maafisa waandikishaji orodha ya wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuzingatia muda wa kufungua   na kufunga vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi pindi wawapo katika maeneo yao ya kazi. “Vituo vyetu kama mlivyotangaziwa vitafunguliwa saa mbili kamili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili jioni. Sasa isije ikatokea ukaona hakuna watu ukaweka vitabu kwenye begi ukaondoka. Sisi tunapita kukagua kila kituo na bahati nzuri kila kata, kila mtaa kuna mtu anayesimamia huo mtaa. Kwahiyo, kuna...

Mradi wa majaribio wa usimamizi taka kuanza Dodoma

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira wanatekeleza mradi wa majaribio wa usimamizi wa taka za plastiki katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kuhamasisha njia bunifu katika usimamizi wa taka za plastiki kupitia dhana ya uchumi rejeshi ili kupunguza taka za plastiki kwenye mazingira na kuboresha maisha na uchumi wa taifakwa ujumla. Baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo uliopo katika Kata ya Chamwino, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Aliy Mfinanga, alisema kuwa mradi wa majaribio utawanufaisha na kuwawezesha jamii na vikundi vya usafi kufanya shughuli za ukusanyaji na usafirishaji wa taka katika Kata ya Chamwino kwa nia ya kutia thamani kupitia dhana ya uchumi rejeshi ili kutunza Mazingira kutokana na plastiki. “Tumeshazoea kuona msisitizo mkubwa kuwa taka ni taka na kwamba haifai tena, lakini kupitia mradi huu wa majaribio tunataka kuonesha jamii kuwa tunaweza kuongeza...

Maafisa Waandikishaji waaswa uadilifu

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Maafisa waandikishaji orodha ya wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameaswa kuwa waadilifu ili Dodoma iwe ya kwanza kwa idadi kubwa ya watu walioandikishwa. Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma, Coletha Kiwale Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma, Coletha Kiwale wakati akizungumza na maafisa waandikishaji, watendaji wa mitaa, wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata pamoja na maafisa watendaji wa kata wakati wa mafunzo kwa maafisa waandikishaji wa orodha ya wapiga kura leo katika ukumbi wa Mtumba Complex jijini Dodoma. Kiwale aliwataka maafisa waandikishaji kuwa weledi na wenye ufanisi katika suala la muda, mavazi na utoaji taarifa kwa wakati. Msisitizo mwingine alisisitiza wawe waadilifu na wahamasishaji kwa waandikishaji kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura. “Napenda tushirikishane ...

Mkoa wa Dodoma kinara Mazingira ya Uwekezaji

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Mkoa wa Dodoma umeibuka kinara kwa kuwa mkoa wa kwanza kupokea tuzo za uwekezeji na utengenezaji wa mazingira wezeshaji ya biashara kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa “Chember of Commerce” (TCCIA) kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 7 Oktoba, 2024. Senyemale alisema kuwa kupokea tuzo hiyo ni heshima kubwa sana na inahamasisha namna ya kuendelea kuboresha mazingira wezeshaji ya biashara kila siku. “Sisi kwa Mkoa wa Dododma tunajua tunazo fursa nyingi lakini pia tunao wafanyabiashara wengi kwa vitengo mbalimbali na tunashukuru kuwa tuzo hizi tunazipata sio kwa Serikali ya Mkoa kusema sisi tunafanya vizuri, Tuzo hizi zinatolewa baada ya wafanyabiashara wenyewe kusema tunaonaje huduma tunazo zipata kutoka serikalini” alisema Senyamule. Aidha, Mwenyekiti wa TCCIA Dodoma, Vivian Komu, alitoa ta...

KADI YA MPIGA KURA SIO LAZIMA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura zoezi litakalofanyika kwa muda wa siku kumi kuanzia tarehe 11- 20 Oktoba, 2024 na kusema kuwa kadi ya mpiga kura siyo kigezo cha kupigia kura. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma alisema hayo alipokuwa akizungumza na mamia ya watumishi wa umma na wananchi waliojitokeza katika Bonanza la kuhamasisha umma kujitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Shule ya Sekondari Dodoma iliyopo Mtaa wa National Housing, Kata ya Makole jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema “hakuna kadi ya mpiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, siku ya kupiga kura unaweza kwenda na kitambulisho chochote kile kama leseni ya udereva, kadi ya mpiga kura ya uchaguzi mkuu, kadi ya bima ilimradi utambulishwe na kadi yoyote. Na kama hauna kabisa basi hata jirani yako anaeaminika kuwa ni mkazi na ana kadi husika anaweza kukutambulisha”. ...

“Maandalizi Uandikishaji Uchaguzi Serikali za Mitaa yamekamilika” Dkt. Sagamiko

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko amesema kuwa maadalizi katika uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika kwa asilimia mia moja. Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko akifafanua jambo Dkt. Sagamiko alitoa kauli hiyo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua Bonanza kubwa la kihistoria la kuhamasisha umma kushiriki mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Msimamizi huyo alisema kuwa maandalizi katika uandikishaji kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yamekamilika. Vifaa vyote vimefika na rasilimali fedha, Rais amewezesha kwa asilimia mia moja. “Kwa maandalizi, tupo timamu. Matamanio yetu tukamilishe zoezi la uandikishaji katika siku tatu” alisisitiza Dkt. Sagamiko. Aidha, aliwapongeza watumishi na wananchi waliojitokeza kwa wingi kushiriki ‘jogging’ n...