Mkoa wa Dodoma kinara Mazingira ya Uwekezaji
Na. Asteria Frank, DODOMA
Mkoa wa Dodoma umeibuka kinara kwa kuwa
mkoa wa kwanza kupokea tuzo za uwekezeji na utengenezaji wa mazingira wezeshaji
ya biashara kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa
“Chember of Commerce” (TCCIA) kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 7 Oktoba,
2024.
Senyemale alisema kuwa kupokea tuzo
hiyo ni heshima kubwa sana na inahamasisha namna ya kuendelea kuboresha
mazingira wezeshaji ya biashara kila siku. “Sisi kwa Mkoa wa Dododma tunajua
tunazo fursa nyingi lakini pia tunao wafanyabiashara wengi kwa vitengo
mbalimbali na tunashukuru kuwa tuzo hizi tunazipata sio kwa Serikali ya Mkoa
kusema sisi tunafanya vizuri, Tuzo hizi zinatolewa baada ya wafanyabiashara
wenyewe kusema tunaonaje huduma tunazo zipata kutoka serikalini” alisema
Senyamule.
Aidha, Mwenyekiti wa TCCIA Dodoma,
Vivian Komu, alitoa taarifa kuwa Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC)
uliyofanyika Ikulu Dar-es-Salaam Julai 29, 2024 na Mkao wa Dodoma kuwa wa
kwanza kupokea tuzo ya kuendesha mabaraza ya biashara.
Alisema kuwa tuzo hiyo ilitokana na Mwenyekiti
wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. “Kwa kusimamia majukumu
ya wafanyabiashara na kusikiliza kero na kuwa mstari wa mbele katika kujitoa
kwenye mabaraza ya biashara na ndio maana tumeweza kupata nafasi hiyo ya kuwa
mshindi wa kwanza kitaifa” alisema Komu.
Nae Katibu Mtendaji wa TCCIA Dodoma,
Ringo Iringo alisema kuwa anampongeza Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa tuzo aliyepewa na
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia
Rosemary Senyamule kama Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa maana amekuwa akijitoa sana kwa
wafanyabiashara. “Mkoa wa Dodoma ulikuwa na changamoto nyingi sana katika
maeneo ya uwekezaji upatikanaji wa viwanja kwaajili ya uwekezaji lakini maeneo
mbalimbali katika sekta binafsi za mkoa wetu. Mkuu wa mkoa amekua wa haraka sana
kufikika lakini pia amekuwa akichajisha na kuhamasisha kufanyika kwa baraza la
biashara” alisema Iringo.
MWISHO
Comments
Post a Comment