Mila na Desturi kandamizi mwiba kwa mtoto wa kike
Na. Faraja Mbise, DODOMA
Tanzania
inaungana na mataifa mengine katika kupambana na changamoto ya mila na desturi
kandamizi ambazo ni kikwazo kwa mtoto wa kike katika kutimiza ndoto zake hasa
katika suala la uongozi.
Akizungumza
katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani yaliyofanywa na Shirika la
Msichana Initiaves, jijini Dodoma, Balozi. Liberata Mulamula alisema kuwa am
tot desturi kandamizi ni kikwazo kwa binti katika kuzifikia ndoto zake hasa
katika uongozi.
Balozi
Mulamula alisema “mila na desturi kandamizi zinamyima mtoto wa kike haki yake
ya msingi ya kwenda shule kusoma. Kwahiyo, zinapunguza idadi ya wanawake kuwa
viongozi. Mila na desturi kandamizi ndani ya jamii zinampa mtoto wa kike
machaguzi machache ambayo yanapelekea kupoteza watoto wa kike wengi sana”.
Aidha,
alisisitiza mtoto wa kike kutumia teknolojia kwa lengo la kujifunza na kuelimika
hasa katika mitandao ya kijamii. Aliwataka waitumie waitumie kwa ufasaha katika
kupata elimu na kuwataka kujitambua na kujiamini katika maisha akisema kuwa ndio
msingi mkuu wa kuwa kiongozi bora.
“Uzuri
wa teknolojia au intaneti haichagui jinsi, haina ubaguzi wa kijinsia, ni jinsi
gani unaitumia kwa manufaa yako, kuongeza ujuzi wako, katika kuleta ustawi wa
jamii na maendeleo ya taifa letu” alisistiza Balozi Mulamula.
Kwa
upande wake Meneja miradi wa Shirika la Msichana Initiatives, Furahini Michael
alizungumzia changamoto nyingi zinazomkwamisha msichana kushiriki katika
kufanya maamuzi na kutaja mila na desturi kandamizi kuwa ni kikwazo kikubwa
sana.
“Mila
na desturi kandamizi ambazo kwa namna moja zinawatoa wasichana kwenye kushiriki
nafasi mbalimbali katika kufanya maamuzi. Mfano katika ngazi ya familia, mtoto
wa kike anakuwa msikilizaji na mtekelezaji tu. Kwahiyo, kutokana na hizo mila na
desturi kandamizi wasichana wameachwa nyuma kwenye masuala ya uongozi” alisisitiza
Furahini.
Hata
hivyo, baadhi ya wadau mbalimbali wa haki za mtoto wa kike wametoa ushauri
kuwa, watoto wa kike watumie teknolojia kwa matumizi sahihi na waishi maisha
yao na sio kufuata maisha ya mitandaoni ambayo yatawapelekea kuua ndoto zao.
Meneja
wa miradi katika Shirika la Plan International, Peter Mwakabwale alisema “kumekuwa
na matumizi mabaya ya kimitandao ambayo imepelekea kuweza kuwepo na unyanyasaji
kwa njia ya teknolojia, wasichana wamekuwa wakijihusisha katika mitandao kwa
lengo ambalo si rafiki”.
Katika
maadhimisho hayo ya siku ya mtoto duniani wadau hao walipata fursa ya kuongea
na watoto wa kike kuhusiana na masuala mbalimnbali yanayohusu teknolojia na kwa
namna gani wataweza kuitumia ili kufikia malengo yao na kuwasisitika kushiriki
katika nafasi za uongozi pindi wawapo shuleni na katika masuala ya kijamii.
Kila
mwaka tarehe 11 Oktoba, Tanzania inaungana na mataifa mengine ulimwenguni
katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani ambapo kaulimbiu kwa kwa mwaka
huu 2024 ni “Msichana na Uongozi, Tumshirikishe Wakati ni Sasa”.
MWISHO
Comments
Post a Comment