Posts

Kata ya Zuzu yajivunia mafanikio ya utekelezaji miradi ya maendeleo

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA SERIKALI yapongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi wa Kata ya Zuzu ikiwa na matokeo chanya. Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah Pongezi hizo zilitolewa na Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Diwani Abdallah alisema kuwa miradi ya ujenzi wa madarasa mapya, visima vya maji na barabara za lami inakwenda sambamba na malengo ya serikali ya kuhakikisha huduma bora kwa wananchi. Miradi hiyo imeanza kutoa matokeo chanya na wananchi wanaendelea kunufaika nayo. "Kwanza tunatekeleza mradi mkubwa wa Kituo cha Afya Zuzu kitakachogharimu shilingi milioni 550 na mpaka sasa takribani shilingi millioni 320 tumeshazipokea na ujenzi unaendelea. Tumejenga madarasa nane, matundu 16 ya vyoo na ofisi za walimu kwa ajili ya kidato cha tano na sita ambao tunatarajia mwaka unaofuatia tutaanza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita. "Lakini pia tunaj...

Diwani Chibago azindua zoezi la ugawaji baiskeli 150 kwa wanafunzi wa Jiji la Dodoma

Image
Na.   Flora    Nadoo, MPUNGUZI Mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhil Chibago amezindua zoezi la ugawaji wa baiskeli 150 kwa wanafunzi wa kike na kiume wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu. Chibago ambae ni Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu alizindua zoezi hilo katika Shule ya Sekondari Mpunguzi iliyopo jijini Dodoma. Mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhil Chibago akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpunguzi baiskeli Diwani Chibago alisema “zoezi hili linahusisha ugawaji wa baiskeli 150 katika shule tano za sekondari za Mkoa wa Dodoma. Baiskeli hizi ili ziishi ni lazima sisi tuzitunze. Hivi si vyombo ambavyo ni kamili, haviwezi kuharibika, vitaharibika. Lakini je ni sahihi kwamba baiskeli ikiwa imepata pancha irudishwe? Jibu ni hapana, kwa sababu hii haijakaa sawa, yale matatizo madogo madogo tunaweza kuyatatua wenyewe. Hivyo, basi kuna msemo unaosema kuwa ukibebwa na wewe bebeka. Shirika h...

CCM yampongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan utekelezaji Ilani

Na. Dennis Gondwe, DODOMA CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, John Mongela alipotoa salamu za CCM katika kilele cha maonesho ya Nanenane kitaifa, Nzuguni Dodoma. Mongela alisema “Ilani ya CCM ina kurasa 308, kurasa 33-56 zinaelezea sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Leo mimi ni shahidi kwamba utekelezaji wa Ilani unafanywa kwa kiwango cha juu sana, tumpongeze Rais na serikali yake. Chini ya uongozi wako ni kazi kubwa inatambulika kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Aidha, aliahidi CCM kuendelea kufanya kazi karibu na serikali ili wananchi wapate maendeleo zaidi. Akitoa salamu kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle alisema kuwa washirika wa maendeleo wanaunga mkono juhudi za Tanzania katika kukuza sekta za Kilimo,...

Jiji la Dodoma kidedea maonesho ya Nanenane 2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kinara wa tuzo na zawadi mbalimbali kwenye maonesho ya kimataifa ya Nanenane kutokana na kufanya vizuri katika maeneo mengi na kuwa kivutuo kwa wageni waliotembelea maonesho hayo. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufungua wa Trekta mkulima Dafalah S. Wadaa, Mkulima bora wa Kanda Kitaifa aliyezawadiwa Trekta na Bodi ya Pamba  Katika tuzo na zawadi zilizotangazwa mbele ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka mshindi katika vipengele sita vya mashindano ya Nanenane. Katika kipingele cha zawadi za wakulima bora kitaifa Kanda ya Kati iliyotolewa na Bodi ya Pamba, Dafalas Wadaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma alizawadiwa zawadi ya Trekta. Kipengele cha wafugaji bora, mshindi wa kwanza aliibuka John Nassar kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuzawadiwa mitamba miwili yenye thamani ya shilingi 9,000,000, mashine ya kukamua yenye thamani ya shilingi 2,300,000 na fedha...

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha Matrekta jijini Dodoma

Image
  Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo kwa lengo la kusogeza matumizi ya matrekta karibu na wakulima nchini na kuwapunguzia gharama. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta Jiwe hilo la msingi liliweka na Rais katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma. Akitoa maelezo ya awali, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema kuwa kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo ni ushirikiano wa kampuni ya Agricom na Mahindra kutoka nchini India. Alisema kuwa makubaliano baina ya wizara yake na Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini, Angelina Ngalula ni kuwa kampuni hizo kufikia mwezi Juni, 2025 kiwanda hicho kianze kutoa huduma. Aidha, kiwanda cha kuunganisha matrekta kinajengwa katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Dodoma eneo lenye ukubwa w...

Jiji la Dodoma lavuka lengo na kukusanya 103% makusanyo ya mapato ya ndani 2023/2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kukusanya fedha za mapato ya ndani shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103 ya lengo la mwaka wa fedha 2023/2024 wakati ikipeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo. Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili-Juni, 2024) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa bajeti ya mapato ya ndani ya mwaka 2023/2024 ilikuwa shilingi 50,097,458,280. Fedha iliyokusanywa ni shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103. Alisema kati ya fedha hizo za mapato ya ndani, asilimia 73.4 ilipelekwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimi...

Ujenzi wa Kituo Kipya cha Afya Chang'ombe kusaidia wananchi zaidi ya 200 kwa siku

Image
Na. John Masanja, CHANG’OMBE Wananchi wa Kata ya Chang’ombe waishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kupunguza kadhia ya upatikanaji wa huduma za afya kupitia ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Chang’ombe.   Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikila akifafanua jambo Akizungumza katika mahojiano maalum na wanahabari, Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Bakari Fundikila alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 500 umekuwa na msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo. Kituo hicho ni msaada pia kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni kwakuwa awali walikuwa wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma za kiafya.   Diwani Fundikila alisema kuwa kwasasa kituo hicho kinaendelea kutoa huduma mbalimbali za kawaida na za kibingwa kwa wananchi. Alisema kuwa kabla ya ujenzi wa kituo hicho huduma hizo walikuwa wakizifuata katika hospitali kubwa zilizo mbali ikiwemo Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.   “Ukienda kutazama taarifa za wagonjwa, utakuta kwa siku kituo h...

Jiji la Dodoma lakusanya 103% mapato ya ndani 2023/2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kukusanya fedha za mapato ya ndani shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103 ya lengo la mwaka wa fedha 2023/2024 wakati ikipeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo. Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi kwa kipindi cha robo ya nne (Aprili-Juni, 2024) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kayombo ambae ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa bajeti ya mapato ya ndani ya mwaka 2023/2024 ilikuwa shilingi 50,097,458,280. Fedha iliyokusanywa ni shilingi 51,402,342,226 sawa na asilimia 103. Alisema kati ya fedha hizo za mapato ya ndani, asilimia 73.4 ilipelekwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimi...

Maendeleo ya Miradi Kata ya Makole

Na. Jackline Patrick, DODOMA Maendeleo ya kata ya makole yanatokana na serikali kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoboresha maisha ya wananchi. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa kata ya Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhusu maendeleo ya kata ya makole. "Maendeleo ya Kata ya Makole yanatokana na miradi ya maendeleo ambayo imeanzishwa. Kata ina miradi mikubwa mingi kuna ujenzi wa madarasa kiwango cha ghorofa, uliogharimu takribani shilingi milioni 500. Tunamiradi tofauti tofauti ili kuweza kukamilisha miradi hiyo lazima kuwe na jitihada" alisema Haji. Vilevile, Kata ya Makole "inaujenzi katika eneo la D center na Ofisi ya wamachinga Jijini Dodoma. Katika maendeleo haya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo pia amechochea miradi kusonga mbele, haisuisui, miradi haina viporo na kukamilika kwa wakati" alisisitiza Haji. ...

Dodoma Jiji FC yaja kivingine

Image
Na. Fadiga James, DODOMA Timu ya Mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji ambayo imekuwa ikishiriki ligi kuu nchini imeweka mikakati mizito kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC premier league) unaotarajia kuanza hivi karibuni.   Mikakati hiyo ilitajwa na Diwani wa Kata ya Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhusiana na maandalizi ya Dodoma Jiji FC kuelekea kuanza kwa ligi kuu. Diwanni Haji alisema kuwa timu hiyo imejiwekea mikakati kwenye msimu mpya wa mashindano unaotarajia kuanza mwisho mwa mwezi Agosti, 2024 kuwa ni kushinda mechi zote. ‘Mimi kama mdau wa Dodoma Jiji FC kwanza najivunia na kujisikia fahari kuwa na timu inayoshiriki ligi kuu. Kwahiyo, cha kwanza wananchi wetu wa Dodoma watafurahia kuangalia mechi kwa timu zinazoshiriki ikiwemo Simba, Yanga na Azam na timu nyingine kwasababu lazima zije kucheza hapa. Sisi kama Dodoma Jiji FC tulikaa wakati tunavunja kambi na Mkurugenz...