Maendeleo ya Miradi Kata ya Makole
Na. Jackline Patrick, DODOMA
Maendeleo ya kata ya makole yanatokana na
serikali kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo
inayoboresha maisha ya wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa kata ya
Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa
mikutano wa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhusu maendeleo ya kata ya makole.
"Maendeleo ya Kata ya Makole yanatokana
na miradi ya maendeleo ambayo imeanzishwa. Kata ina miradi mikubwa mingi kuna ujenzi
wa madarasa kiwango cha ghorofa, uliogharimu takribani shilingi milioni 500. Tunamiradi
tofauti tofauti ili kuweza kukamilisha miradi hiyo lazima kuwe na
jitihada" alisema Haji.
Vilevile, Kata ya Makole "inaujenzi katika
eneo la D center na Ofisi ya wamachinga Jijini Dodoma. Katika maendeleo haya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo pia amechochea miradi
kusonga mbele, haisuisui, miradi haina viporo na kukamilika kwa wakati" alisisitiza
Haji.
Kata ya Makole zilitolewa fidia kwa
wananchi wapatao sita katika eneo la ‘D center’ Makole ambao wameshalipwa zaidi
ya shilingi milioni sita pamoja na miradi mingi ya serikali ya kimikakati.
Diwani huyo aliongeza kwa kusema kuwa
alianzisha Diwan Cup katika Kata ya Makole kwa sababu kata hiyo ipo vizuri
kimichezo.
Habari hii mehaririwa na Emmanuel Lucas
MWISHO
Comments
Post a Comment