Jiji la Dodoma kidedea maonesho ya Nanenane 2024
Na.
Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI
ya Jiji la Dodoma kinara wa tuzo na zawadi mbalimbali kwenye maonesho ya
kimataifa ya Nanenane kutokana na kufanya vizuri katika maeneo mengi na kuwa
kivutuo kwa wageni waliotembelea maonesho hayo.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufungua wa Trekta mkulima Dafalah S. Wadaa,
Mkulima bora wa Kanda Kitaifa aliyezawadiwa Trekta na Bodi ya Pamba
Katika
tuzo na zawadi zilizotangazwa mbele ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka mshindi katika vipengele sita vya mashindano
ya Nanenane.
Katika
kipingele cha zawadi za wakulima bora kitaifa Kanda ya Kati iliyotolewa na Bodi
ya Pamba, Dafalas Wadaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma alizawadiwa zawadi
ya Trekta.
Kipengele
cha wafugaji bora, mshindi wa kwanza aliibuka John Nassar kutoka Halmashauri ya
Jiji la Dodoma na kuzawadiwa mitamba miwili yenye thamani ya shilingi 9,000,000,
mashine ya kukamua yenye thamani ya shilingi 2,300,000 na fedha taslimi
shilingi 18,700,000.
Maeneo
mengine ambayo Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibika kidedea ni eneo la
wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa ambapo wafugaji John Nassar aliibuka mshindi
wa kwanza na kupata zawadi ya shilingi 2,500,000 na Viola Kweka, mshindi wa pili
na kupata zawadi ya shilingi 2,000,000. Kwa wafugaji wadogo wa mbuzi wa nyama,
Venderine Liakurwa pia wa Dodoma Jiji aliibuka mshindi wa pili na kupata zawadi
ya shilingi 1,000,000.
Eneo
la wafugaji wadogo wa mbuzi wa maziwa, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilitoa
washindi wa kwanza na wa pili mtawalia. John Nassari aliyepata zawadi ya
shilingi 1,500,000 na Caroline Shayo aliyepata shilingi 1,000,000.
Kwa
washindi katika mikoa ya Dodoma na Singida, Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliibuka
kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza ikizitangulia Halmshauri za Wilaya ya Kondoa
na Mpwapwa za Mkoa wa Dodoma.
Maonesho
ya Nanenane mwaka 2024 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Chagua viongozi bora
wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
MWISHO
Comments
Post a Comment