Dodoma Jiji FC yaja kivingine
Na. Fadiga James, DODOMA
Timu
ya Mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji ambayo imekuwa ikishiriki ligi kuu nchini
imeweka mikakati mizito kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC
premier league) unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Mikakati
hiyo ilitajwa na Diwani wa Kata ya Makole, Omary Haji alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhusiana
na maandalizi ya Dodoma Jiji FC kuelekea kuanza kwa ligi kuu.
Diwanni
Haji alisema kuwa timu hiyo imejiwekea mikakati kwenye msimu mpya wa mashindano
unaotarajia kuanza mwisho mwa mwezi Agosti, 2024 kuwa ni kushinda mechi zote.
‘Mimi
kama mdau wa Dodoma Jiji FC kwanza najivunia na kujisikia fahari kuwa na timu
inayoshiriki ligi kuu. Kwahiyo, cha kwanza wananchi wetu wa Dodoma watafurahia kuangalia
mechi kwa timu zinazoshiriki ikiwemo Simba, Yanga na Azam na timu nyingine
kwasababu lazima zije kucheza hapa. Sisi kama Dodoma Jiji FC tulikaa wakati
tunavunja kambi na Mkurugenzi wa Jiji, mkurugenzi ana mikakati mingi sana
mizuri na nina imani kabisa Dodoma Jiji FC itafanya vizuri msimu huu kwasababu
tuna malengo madhubuti sana ili kuhakikisha Dodoma Jiji FC inafanya vizuri. Mechi
zote za Dodoma za nyumbani inatakiwa tushinde ili tujiweke katika nafasi nzuri
pamoja na mechi za ugenini’’ alisema Haji.
Pia
licha ya mikakati na mpango mzuri kuelekea msimu mpya wa mashindano ambao ni
kushinda mechi zake za nyumbani lakini Dodoma Jiji FC imeonekana kuwa na
matokea mazuri kipindi hiki cha maandalizi ambapo timu iliweka kambi jijini
Arusha. Kati michezo minne ya mwisho Timu ya Dodoma Jiji FC ilifanikiwa kuibuka
na ushindi katika michezo yote huku ikitoshana nguvu katika mchezo mmoja na
Fountain Gate FC.
Timu
ya Dodoma Jiji FC imekuwa na muendelezo mzuri katika ligi kuu ya NBC ikiwa ni zaidi
ya misimu mitatu sasa ikisalia katika ligi hiyo na kuendelea kutoa ushindani
mzuri hususani kwa timu ambazo madaraja yao yanalingana.
Habari
hii imehaririwa na Emmanuel Lucas
Comments
Post a Comment