Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha Matrekta jijini Dodoma
Na.
Dennis Gondwe, DODOMA
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la
msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo kwa lengo la
kusogeza matumizi ya matrekta karibu na wakulima nchini na kuwapunguzia gharama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi kiwanda cha kuunganisha matrekta
Jiwe hilo la msingi liliweka na Rais katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Akitoa
maelezo ya awali, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema kuwa kiwanda cha
kuunganisha matrekta na zana nyingine za kilimo ni ushirikiano wa kampuni ya
Agricom na Mahindra kutoka nchini India. Alisema kuwa makubaliano baina ya
wizara yake na Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi nchini, Angelina Ngalula ni
kuwa kampuni hizo kufikia mwezi Juni, 2025 kiwanda hicho kianze kutoa huduma.
Aidha,
kiwanda cha kuunganisha matrekta kinajengwa katika viwanja vya Nanenane,
Nzuguni Dodoma eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takribani mita za mraba 20,000
kikiunganisha matrekta aina na Swaraj na kutarajiwa kuzalisha ajira za kudumu
400 na ajira zisizo za kudumu zaidi ya 2000.
Ikumbukwe
kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho ni matokeo ya ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan nchini India na kualika wawekezaji wa India kuwekeza nchini Tanzania pamoja
na mambo mengine.
MWISHO
Comments
Post a Comment