Posts

Ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu wafikia 98%

Image
Na. Dennis Gondwe, ZUZU UJENZI wa Kituo cha Afya Zuzu umefikia asilimia 98 ya utekelezaji kikitarajiwa kuhudumia wananchi 10,054 kwa kuwahakikishia huduma bora za afya na kuwaondolea hadha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya. Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Goodluck Magoti alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Magoti alisema “kutokana na changamoto ya kukosa huduma za Kituo cha Afya katika Kata ya Zuzu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilianza ujenzi wa Kituo cha Afya Zuzu ili kusogeza huduma za matibabu mbalimbali karibu na wananchi. Halmashauri ilitoa kiasi cha shilingi 299,439,348,54. Hadi kufikia sasa kiasi cha shilingi 285,4439,000,54 zimetumika kwa ujenzi wa majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na Maabara na kubakiwa na shilingi 14,000,348.54 kwa ajil...

DC Shekimweri ahimiza usafi kudhibiti magonjwa Dodoma

Image
  Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri aliitaka jamii kuzingatia suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujikinga na magonjwa na kufanya mji kuwa safi na salama katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti ya halmashauri ili wananchi wawe na afya bora. Aliyasema hayo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupokea na kujadili mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2025/2026. Alhaji Shekimweri alisema “ wenzetu maafisa afya, watendaji wa kata, changamoto za uchafu wa mji wetu ni usimamizi kwa sehemu fulani, yapo maeneo ya kampuni za usafi, yapo maeneo yanavikundi vya usafi, lakini ni wajibu wa mwananchi mmoja mmoja kufanya usafi wa eneo lake. Kwahiyo, tuimarishe usimamizi, na kuna makampuni na vikundi na vinalipwa kwa kufanya kazi hizo ” . Akiongelea suala la usalama katika Halmashauri y...

Dodoma Jiji U-20 yakita Kambi Kileleni

Image
Na. Mussa Richard, DODOMA Klabu ya soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 (U-20) imeendeleza ubabe kwa wapinzani wake wanaoshiriki ligi ya vijana ya NBC chini ya umri wa miaka 20 Tanzania bara baada ya kuwashushia kichapo cha mabao 2-1 wanajeshi wa mpakani Mashujaa FC U-20, katika mchezo uliovulumishwa katika nyasi za dimba la Jamhuri Dodoma hapo jana. Baada ya mchezo kutamatika kocha wa Dodoma Jiji U-20, Jeremiah Chido alisema “ mchezo umemalizika salama na tumepata kitu ambacho tulikua tunakihitaji ambacho ni alama tatu muhimu. Alama ambazo zinatufanya tuendelee kuwa kileleni katika kundi letu na kutufanya tusicheze kwa presha michezo inayokuja mbele yetu, michezo ambayo tutakuwa ugenini ”. Katika hatua nyingine Chido akaweka wazi malengo yao kwenye msimu huu wa Ligi ya Vijana ya NBC Tanzania Bara. “ Malengo yetu msimu huu ni kuchukua ubingwa kwasababu msimu uliopita tulifika fainali ila bahati haikuwa upande wetu. Kwahiyo, msimu huu tukishirikiana halmashauli, mashabiki...

Prof. Mwamfupe; Taka ni fursa ya kutengenezea mbolea

Image
  Na. Aisha Haji, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na kutumia takataka zinazotokana na mazao kama fursa ya kutengeneza mbolea ili kuweza kuinua sekta ya kilimo na uchumi wa halmashauri kiujumla. Aliyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa majadiliano na Kamati ya Ushauri ya Wilaya iliyokutana kupitia mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Akizungumza kuhusu umuhimu wa mbolea zitokanazo na takataka za mazao, alisema kuwa taka za mazao ambazo zinaoza kwa urahisi ni fursa nzuri sana ya kiuchumi kuweza kutengeneza mbolea. Pia alidokeza kuwa halmashauri imejipanga katika suala la kutoa mikopo, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa wananchi kuhusu namna ya kutumia taka zitokanazo na mazao kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kuku kwa kufuata utaratibu maalumu. Prof. Mwamfupe alisema “halmashauri itak...

Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa NeST kwa Walimu Wakuu Jiji la Dodoma

Image
 

Walimu wakuu Jiji la Dodoma kupatiwa Mafunzo ya NeST

Image
Na. Faraja Mbise, DODOMA Walimu wakuu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamepatiwa mafunzo juu ya ununuzi kwa njia ya mtandao serikalini yatakayoboresha utendaji kazi na kuwawezesha kupata mafundi na watoa huduma kupitia mfumo wa ununuzi ‘ National e-Procurement System of Tanzania’ yaani ‘NeST’. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero akifungua Mafunzo ya Ununuzi kwa njia ya Mtandao (NeST)  Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 21 Januari, 2025 na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi cha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa walimu wakuu wa shule za msingi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Vincent Odero alisema kuwa mfumo wa manunuzi serikalini kwa njia ya kielektroniki ni mfumo mzuri na umerahisisha mchakato mzima wa manunuzi na umeleta ufanisi mkubwa katika ununuzi wa umma katika maeneo mbalimbali. “Mfumo huu ni mzuri, umerahisisha ...

Nyuki wa Tabora walamba Zabibu Sita

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Timu ya mpira wa miguu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji yainyuka goli 6-0 timu ya mpira wa miguu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 ya Tabora United ndani uwanja wa Jamhuri Jiji la Dodoma katika mechi ya kwanza mzunguko wa pili wa ligi ya NBC Youth League 2024/2025. Kocha wa timu ya vijana umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji FC, Chido Jeremia alisema hawakuwa na mchezo mzuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili walikuwa na nyakati nzuri kwa jinsi vijana walivyowaelekeza kwa hali ya kuona mapungufu ya wenzao na kuweza kupata magoli hayo. Alisema kuwa timu inaendelea kuimarika na malengo waliyowawekea yanazidi kupungua maana kadri siku wanavyocheza mechi wanapata alama. “Vijana wametuheshimisha tumepata ushindi na sio tu matokeo mazuri ila matokeo yenye magoli mengi kama vile tulivyokuwa tunataka maana tulikuwa tunataka kutengeneza ‘margin’ nzuri zaidi ya wanaotufata lakini pia kutengeneza ‘goal difference’ ambayo ndio vijana wametu-off...

Dodoma Jiji U20 yatuma salamu Ligi ya Vijana

Image
Na Mussa Richard, DODOMA   Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji chini ya umri wa miaka 20 imetuma salamu kwa timu zinazoshiriki ligi ya vijana ya NBC chini ya miaka 20 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Tabota United chini ya miaka 20 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma hapo jana. Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha mkuu wa timu hiyo, Chido Jeremiah alisema “tunamshukuru Mwenyezi Mungu mchezo umeisha salama na tumepata ushindi wa magoli mengi na ushindi wa kutuheshimisha na kutuweka mbele zaidi na wanaotufuata. Japo hatukua na mchezo mzuri kipindi cha kwanza lakini wakati wa mapumziko tukawapa vijana maelekezo ya kufanya kutokana na mapungufu tuliyoyaona kwa wapinzani wetu ndiyo maana tuliporudi kipindi cha pili tukafanikiwa kupata mabao manne. Kwa upande wa timu imeendelea kuimarika na vijana wameanza kujituma na niwashukuru mashabiki wamejitokeza kuiangalia timu yao na wameona jinsi inavyocheza. Kwahiyo, niwaombe wanadodoma wasiiache timu hii timu ni ...

Kambi: Watoto wenye mahitaji maalum wanahaki ya kusoma

Image
Na. Coletha Charles, CHANG’OMBE Kata ya Chang’ombe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imebainisha na kuwaandikisha watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 kwa kushirikiana na wazazi, walezi na walimu.   Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Issa Kambi akifanya uchunguzi mwanafunzi mwenye mahitaji maalum Akizungumza wakati wa uandikishaji wa watoto hao, Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Issa Kambi, alisisitiza kuwa jukumu la kuwapatia watoto hao fursa ya kusoma lipo mikononi mwa wazazi na walezi kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kwa kuwajengea msingi bora wa maendeleo.   Alisema kuwa, serikali imejipanga kuwahudumia watoto wenye mahitaji maluum kwa kuwapokea na kuwapa mahitaji stahiki na kuhakikisha wanapata nafasi bila kujali changamoto zao. “Wazazi ukiwa na mtoto usichoke kumlea, ukiona umechoka basi huyo mtoto amefanikiwa na tusiwakatie tamaa. Watot...

Elimu ni haki ya watoto wenye mahitaji maalum Kata ya Ipagala

Image
Na. Coletha Charles, IPAGALA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea na jitihada ya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum kiafya kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 katika Kata ya Ipagala. Akizungumza wakati zoezi hilo, Afisa Elimu wa Kata ya Ipagala, Veronica Mpanda, aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum shule kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kulingana na sera ya elimu jumuishi kwa kuwa miundombinu imara ipo kwa ajili yao. Alisema kuwa zoezi hilo linalenga kutambua idadi na aina ya mahitaji ya watoto hao ili kuweka mipango madhubuti ya kuwahudumia. “Zoezi hili la uandikishaji lilitakiwa lifanyike katika Shule ya Msingi ya Ipagala B, lakini hatujafanikiwa kupata mtoto hata mmoja mwenye mahitaji maalum japo zoezi hili ni endelevu na tunatambua kwamba elimu ni haki ya kila mtoto na kupitia zoezi hili tutahakikisha kuwa hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa sababu ya changamoto yoyote” alisema Mpanda. ...