Nyuki wa Tabora walamba Zabibu Sita
Na. Asteria Frank, DODOMA
Timu
ya mpira wa miguu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji yainyuka goli
6-0 timu ya mpira wa miguu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 ya Tabora
United ndani uwanja wa Jamhuri Jiji la Dodoma katika mechi ya kwanza mzunguko
wa pili wa ligi ya NBC Youth League 2024/2025.
Kocha
wa timu ya vijana umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji FC, Chido Jeremia alisema
hawakuwa na mchezo mzuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili walikuwa na
nyakati nzuri kwa jinsi vijana walivyowaelekeza kwa hali ya kuona mapungufu ya
wenzao na kuweza kupata magoli hayo.
Alisema
kuwa timu inaendelea kuimarika na malengo waliyowawekea yanazidi kupungua maana
kadri siku wanavyocheza mechi wanapata alama. “Vijana wametuheshimisha tumepata
ushindi na sio tu matokeo mazuri ila matokeo yenye magoli mengi kama vile
tulivyokuwa tunataka maana tulikuwa tunataka kutengeneza ‘margin’ nzuri zaidi
ya wanaotufata lakini pia kutengeneza ‘goal difference’ ambayo ndio vijana wametu-offer.
Na tunawashukuru mashabiki hawakuwa nyuma kwa kuja kuwasapoti vijana wao na
wanaona wanavyocheza. Vijana hawa sio wa kwetu peke yetu na jukumu la kuwalea
lisibaki kwa halmashauri peke yake au makocha wao ila libaki kwa kila mwana
Dodoma aone wivu kuwa ni sehemu ya chagizo kuwa vijana hawa niliwaleo na huku
ndipo tunapata wachezaji wazuri watakao kuja kutusaidia Dodoma” alisema Chido
Nae
Nahodha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Dodoma Jiji FC, Bakari
Mondwe alisema kuwa wanamshukuru Mungu wamemaliza mchezo wao salama na malengo
yao katika mzunguko huu wa pili ni kuzidi kufanya vizuri ili waweze kuvuka
hatua hiyo. “Tunawaomba mashabiki wazidi kuja kwa wingi na kusapoti timu yao
ili tuzidi kufanya vizuri na tunawaahidi hatutawaangusha na kuwapa kitu muhimu
ambacho wanakuja kukiona kila siku wanapokuja na tutazidi kufanya vizuri”
alisema Mondwe.
Mzunguko
wa pili ulianza tarehe 15 Januari, 2025 ambapo Dodoma Jiji FC wanaongoza ligi,
msimamo wa kundi ‘A’ katika mzunguko wa kwanza wakifuatiwa na Azam FC kwa
nafasi ya pili na Kagera Sugar nafasi ya tatu na nafasi ya nne kushikiliwa na Yanga.
MWISHO
Comments
Post a Comment