Kanda Namba Mbili yaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi
Na. Tutindaga Nkwindi, NZUGUNI Kanda Namba Mbili inayohudumia kata tano za Nzuguni, Ipagala, Ihumwa, Mtumba na Kikombo imeendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kila mkazi wa kanda hiyo anapata huduma kwa wakati na kwa kiwango kinachostahili. Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Kanda hiyo, Abeid Msangi alisema kuwa kanda imejipanga vizuri katika kusimamia utoaji wa huduma kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, ubunifu na uwajibikaji. “ Tunaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haraka na kwa ubora. Tumeweka mifumo ya ufuatiliaji wa maombi ya wananchi na kuboresha mawasiliano kati ya ofisi na jamii ili kuongeza ufanisi ” alisema Msangi. Aidha, alieleza kuwa maafisa walioko katika kanda hiyo wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya mara kwa mara kuhusu utoaji wa huduma kwa wateja na matumizi ya teknolojia katika kushughulikia maombi ya wananchi, hatua ambayo imepunguza changamoto za ucheleweshaji wa huduma. Vilevile, alisisi...
Comments
Post a Comment