Huduma bora ni msingi wa kazi Kanda Namba Tatu
Na. Mwandishi Wetu, KIZOTA
Kanda Namba Tatu yaonesha kiwango bora cha huduma kwa
wateja kwa kuendelea kufanya vizuri katika kutoa huduma zinazogusa matarajio ya
wananchi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Kanda Namba Tatu ya utoaji huduma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fanuel Lawrence alipokuwa akiongelea Wiki ya Huduma kwa Mteja katika kanda hiyo. Alisema kuwa huduma bora ni wajibu wa kila mtumishi wa umma na njia ya kuj
enga imani na uaminifu wa
wananchi kwa serikali yao. “Huduma bora ni msingi wa kazi yetu, tunapaswa kuwa
na mbinu mpya, kuwa na adabu, na kujitolea ili wananchi wapate huduma stahiki” alisema
Lawrence. Aidha, aliwakaribisha wananchi na wafanyabiashara katika ofisi ya Kanda
Namba Tatu zilizopo katika pamoja na Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kizota kupata
huduma zote muhimu. Aliongeza kuwa ofisi hizo zimesogezwa karibu na wananchi
ili kuwapunguzia kero ya kufuata huduma mbali na makazi na shughuli zao.
Nae, Afisa Biashara wa Kanda Namba Tatu, Steven Maufi
alibainisha kuwa Wiki ya Huduma kwa Mteja ni fursa ya kuhudumia wananchi kwa
namna ya tofauti ili kupata maoni na ushauri kutoka kwao ya namna ya kuboresha
huduma zaidi. “Mbinu zetu za kutoa huduma bora za kiwango cha juu zinategemea
pia maoni ya wateja. Lengo kuu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na
kwa haraka na serikali inapata kile kinacjostahili kwa wakati” alisema.
Kwa upande wake, Mfanyabiashara kutoka Kata ya Nala,
Salehe Hamisi alitoa pongezi kwa kanda hiyo kutoa huduma nzuri. “Mabadiliko ni
makubwa sana, sasa hivi ndugu mwandishi, tunahudumiwa vizuri sana. Hata lugha
wanayotumia ni nzuri tofauti na kipindi cha nyuma, unamkuta mtumishi kwenye
meza ya huduma, anakuhudumia kama ni vita. Sasa hivi wanatupokea vizuri na
wanahakikisha unaondoka umepata kile umekifuata na ukiwa umeridhika” alisema.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yanayofikia
kilele tarehe 10 Oktoba, 2025 yakilenga kuimarisha uhusiano mzuri kati ya taasisi
na wanufaika wa huduma.
Comments
Post a Comment