Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi
Na. Leah Mabalwe, NALA
Ujenzi wa mradi wa Maji Nala unaotekelezwa na
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa gharama ya
shilingi bilioni 1.3 kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika
Kata ya Nala.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Nala, Herman Masila alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Nala.
“Nichukue nafasi hii kuishukuru serikali
kutuletea mradi wa maji katika Kata ya Nala. Mradi huu utasaidia sana wananchi
kuondokana na adha ya maji. Mradi huu ni mkubwa utasaidia maeneo mbalimbali
katika kata yetu inayokuwa kwa kiasi. Kwa siku za usoni tumeshuhudia idadi kuwa
ya watu wanakuja kujenga makazi na viwanda. Hivyo, mradi huu utakapo kamilika
utasaidia kwa kiasi kikubwa na kupunguza adha ya maji” alisema Masila.
Nae, Mary Kaka ambae ni mkazi wa Kata ya Nala aliipongeza
serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kupeleka maendeleo katika Kata ya Nala
na kumshukuru rais kwa kuwajengea mradi wa maji kwasababu utawasaidia kutokana na
ukosefu wa maji.
“Tulikuwa tunapata shida sana kwasababu ya ukosefu wa maji, tulikuwa tukitoka sehemu ya mbali na kufuata maji sehemu nyingine. Lakini ninaamini mradi huu wa maji utakapokamilika usumbufu na ukosefu wa maji katika kata yetu utapotea kabisa” alisema Kaka.
MWISHO
Comments
Post a Comment