Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala
Na. Leah Mabalwe, NALA
Shule
ya Sekondari Nala imefanikiwa kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi
kutokana na utekelezaji wa dhamira ya serikali ya awamu ya sita wa kuhakikisha
wanafunzi wanapata huduma ya chakula na lishe shuleni.
Kauli
hiyo ilitolewa na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nala, Mwl. Joseph Chambo alipokuwa
mwenyeji wa waandishi wa habari waliotembelea shule yake kuona utekelezaji wa
miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni hapo katika
kipindi cha miaka minne ya serikali.
“Katika
utekelezaji wa Muongozo wa kitaifa wa ulaji wa huduma ya chakula na lishe kwa
wanafunzi wa elimumsingi umetunufaisha sana. Hapo awali kulikuwa na mahudhurio hafifu
sana shuleni kwetu. Pia hata tukiwa darasani wanafunzi walikuwa na uelewa wa
chini na hata ufaulu ulikuwa sio mzuri sana. Kufuatia utelekezaji wa mwongozo
huu shule yetu sasa imekuwa ni ya mfano. Watoto wanahamasika kuja shule na hata
ufaulu umepanda kwa kiasi kikubwa kulinganisha na hapo awali. Sisi kama walimu
tumetekeleza muongozo huo kwa kiasi kikubwa sana’’ alisema Mwl. Chambo.
Vilevile,
aliongeza kuwa utoaji wa huduma ya chakula na lishe shuleni hapo ulisaidia
kuepusha vishawishi kwa wanafunzi hasa wanafunzi wa kike. “Huduma ya chakula na
lishe imesaidia kuchochea wanafunzi kuja shuleni na kusoma kwa amani na utulivu
huku wakifuatilia vipindi kwa umakini, jambo lililopelekea kupanda kwa kiwango
cha ufaulu” alisema Mwl. Chambo.
Nae, Mwanafunzi
Vanessa Fidelis aliishukuru serikali kwa utaratibu wa utoaji wa huduma ya
chakula na lishe shuleni hapo.
“Naishukuru
sana serikali kwa kuleta huduma hii shuleni kwasababu imesaidia kuhamasisha
wananfunzi kupunguza utoro na imesaidia kusoma kwa muda mrefu hasa vipindi vya
jioni. Utaratibu huu umesaidia kukuza taaluma yetu na kupandisha kiwango cha
ufaulu” alisema Fidelis.
MWISHO
Comments
Post a Comment