Maeneo ya Shule kupimwa Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,
Alhaj Jabir Shekimweri ameagiza maeneo yote ya shule yapimwe na kupatiwa hati
miliki ili kuepuka migogoro ya Ardhi inayotokana na uvamizi wa mipaka ya shule.
Alhaj Shekimweri aliagiza
maeneo ya shule yaliyopo sasa yapimwe na kutengenezewa hati miliki. Alisema
kuwa utekelezaji huo utasaidia kuepusha migogoro ya Ardhi inayosababishwa na
wananchi kuvamia maeneo ya shule.
Aidha, alishauri ujenzi wa
shule katikati ya mji ujielekeze kwenye majengo ya maghorofa ili katika eneo
dogo litumike vizuri. “Nichukue nafasi hii kuwashukuru wenzetu wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA) wameanza kutuunga mkono. Lakini pia mapato ya ndani ya
halmashauri wameanza kufanya hivyo” alisema Alhaj Shekimweri.
MWISHO
Comments
Post a Comment