Wadau wa Elimu kukutana ngazi ya chini
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewashauri wadau wa elimu wa Halmashauri
ya Jiji la Dodoma kuwa vikao hivyo viwe vinaanzia ngazi ya mitaa na kata ili
wananchi wengi waweze kushiriki katika maendeleo ya sekta ya elimu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akisisitiza jambo |
Ushauri huo aliutoa katika
kikao cha wadau wa elimu Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika
ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper iliyopo jijini Dodoma.
Prof. Mwamfupe alisema
“nilidhani kwamba siku kama leo tutambue kwamba changamoto zinazotukabili
katika sekta ya elimu ni za kienyeji zaidi (localized) ziko zaidi katika maeneo
husika. Kama ndivyo, ili vikao vya wadau wa elimu viwe endelevu tuvishushe
kutoka ngazi hii hadi katika maeneo yetu tukawape watu uhuru wa kuongea ili
siku kama ya leo watu waje na mifano ya vikao katika maeneo mengi zaidi.
Mchakato huu ni muhimu kuanzia ngazi za chini zaidi ambapo tunawafahamu watu
hata wachangiaji kwa majina na tunawafahamu watoro kwa majina”.
MWISHO
Comments
Post a Comment