BenPaul achangia Elimu Dola 300

 

Na. John Masanja, MIYUJI

Dola 300 za BenPaul kwenda kuunga mkono jitihada za elimu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Mfuko la Lishe.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bernard Paul alimaarufu BenPol amechangia kiasi cha dola 300 za kimarekani ikiwa ni ushiriki wake katika kuunga mkono jitihada za elimu ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Msanii BenPol alichangia kiasi hicho wakati wa kikao cha wadau wa Elimu na utoaji wa tuzo za kitaaluma kilichoandaliwa na Ofisi ya Halmashauri Jiji la Dodoma na kufanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper jijini Dodoma.

“Nitoe wito na ombi kwa wazazi, walimu na wadau wote, tuendelee kuwaunga mkono vijana wetu kwenye elimu lakini pia tusiwakataze wanapopenda kufanya sanaa kwasababu vyote viwili vinalipa. Elimu inalipa na sanaa ni ajira” alihitimisha BenPol.

Sanjari na hayo msanii BenPol aliteuliwa na wajumbe wa kikao hicho kuwa Balozi wa Mfuko wa Lishe ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuahidi kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Comments

Popular Posts

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Waziri Mchengerwa apongeza usimamizi wa miradi jijini Dodoma

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma