Walimu Dodoma waaswa uzalendo
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WALIMU wa Halmashauri ya
Jiji la Dodoma wametakiwa kutanguliza uzalendo katika kazi zao ili kuwafundisha
wanafunzi na kuwasaidia katika kujenga taifa lao.
Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Christian Mauya alipochangia katika kikao cha wadau wa elimu |
Kauli hiyo ilitolewa na
Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Christian Mauya alipochangia
katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya St. Gasper jijini Dodoma.
Mauya alisema “mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, mimi binafsi Ndugu zangu walimu nataka kuzungumzia
kipengele cha pili, kipengele cha uzalendo. Sisi, walimu tunakubaliana kabisa
tunakutana na changamoto nyingi sana, lakini nilikuwa naomba sana tuishi katika
uzalendo wetu, uzalendo Tanzania. Hautakaa sehemu yeyote katika maisha yako
yawe yamenyooka, uzalendo kwanza, hebu pigania Tazania yako”.
Aliwakumbusha kuwa wapo
makao makuu Dodoma kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi. “Niwakumbushe kuwa
mmeletwa makao makuu kuhakikisha wanafunzi wa Dodoma wanapata elimu na
wanafaulu, hebu kaa katika eneo hilo ili kuacha alama kwa kazi unayofanya.
Serikali inatuhangaikia sana na inatujali sana, hebu na sisi tuangalie nafasi
yetu ni nini kwenye ile dhamana tuliyopewa” alisema Mauya.
Akiongelea changamoto ya
miundombinu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa yatapungua kwa
kiwango kikubwa. “Nikupongeze wewe mheshimiwa mkuu wa wilaya, raia namba moja
katika Wilaya ya Dodoma. Wakati watu wanawasilisha kulikuwa na hoja ya
miundombinu ya madarasa, madawati, vyoo, ofisi za walimu, nyumba za walimu na
hosteli, walimu oyee!, walimu safii!. Mheshimiwa mkuu wa wilaya kwetu haya ni
maelekezo. Sisi kama Divisheni ya Mipango na Uratibu na mimi kama Mchuni ni
kuhakikisha matatizo hayo tunayapunguza kwa kiwango kikubwa” alisema Mauya kwa
kujiamini.
MWISHO
Comments
Post a Comment