Prof. Mwamfupe apongeza wadau wa elimu
Na.
John Masanja, MIYUJI
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe awapongeza wadau wa
elimu kwa jitihada zao kwenye kukuza sekta ya elimu na kuchangia ufaulu wa
wanafunzi.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe |
Pongezi
hizo alizitoa kwa walimu, wazazi na wadau mbalimbali wa elimu kwa ushirikiano
mzuri katika kukuza na kuinua sekta ya elimu ndani ya Jiji la Dodoma kwenye
kikao cha wadau wa elimu na utoaji tuzo za kitaaluma kilichofanyika katika
ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper jijini Dodoma.
“Natambua
sana kuna changamoto nyingi ambazo mnakutana nazo wakati wa utendaji kazi wenu
lakini hamjawahi kutuangusha na haya mafanikio tunayoyaona sasa hivi katika elimu
ni matunda ya uwekezaji wa pamoja” alisema Prof. Mwamfupe.
Vilevile,
alipendekeza kufanyika kwa vikao vya wadau wa elimu kuanzia ngazi za chini
ambako watu wengi hufikiwa katika kutoa ushauri na kuona namna gani mawazo yao
yatakuwa na manufaa katika kuleta mabadiliko ya elimu kiujumla ndani ya Jiji la
Dodoma.
Kwa
upande wake mlezi wa taaluma kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Justine Machela,
ambaye pia ni Afisa Taaluma wa Mkoa wa Dodoma alisema kuwa uwajibikaji ni moja ya
nguzo ya kuinua ubora wa elimu na ufaulu Dodoma. Akinukuu kutoka kwenye wimbo
ulioimbwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma wakati wa kikao hicho na
hivyo, kuwataka kila mmoja kwenda kuwajibika ipasavyo kwa matokeo chanya ya kielimu
ndani ya Jiji la Dodoma. “Jiji la Dodoma na vitu vyake vyote, vinatakiwa kuendana
na hadhi ya makao makuu ya nchi, chama na serikali” alisema Machela.
Comments
Post a Comment