Posts
Kata ya Chamwino kuanza ujenzi Mabweni Chinangali Sec
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Ujenzi wa Barabara yenye urefu wa kilomita 1.6 fursa kwa wananchi wa Kata ya Nala
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Leah Mabalwe, NALA Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilitenga kiasi cha shilingi 2,431,050,561 kutoka mapato ya ndani kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwaajili ya mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Hospitali ya Jiji mpaka barabara ya Singida yenye urefu wa kilomita 1.6 kwa kiwango cha lami. Hayo yalibainishwa na Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella alipokuwa akisoma taarifa ya ujenzi wa Barabara hiyo kwa Kamati ya Fedha na Utawala iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025. “Ujenzi huu wa barabara unajumuisha daraja kubwa la midomo mitatu pamoja na mingine minne ya duara. Pia utasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi ukizingatia katika barabara hii baadhi yao wanatoka sehemu mbalimbali kwaajili kufuata huduma za afya katika Hospitali ya Jiji na hii itarahisisha kutokana na miundombinu mizuri ya barabara na kuzifikia huduma za afya kirahisi” alisema Mhandisi Bella. Pia alitoa shukrani kw...
Ofisi ya Kata Zuzu yaboreshwa kwaajili ya utoaji huduma bora
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Leah Mabalwe, ZUZU Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania i me lenga kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wa tumishi wa serikali ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi . Hayo yalibainishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Zuzu, Shakila Mwanyemba, alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ndani ya robo ya tatu 2024/2025 wakati wa ziara iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala katika Kata ya Zuzu. “Serikali ya awamu ya sita ilitenga kiasi cha shilingi 15,000,000 kwaajili ya ukarabati wa Ofisi ya Kata ya Zuzu, ikiwa ni chachu ya kuboresha mazingira bora kwaajili ya watumishi ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Pia ofisi hii siyo tu kwaajili ya watumishi pekee, bali hata wananchi wanaweza kuja kupata huduma bora katika ofisi hii kutokana na mazingira ya ofisi kuwa bora, salama na rafiki” alisema Mwanyemba. Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendelea kuboresha utawala bora na kuwas...
‘Team Aprili’ wapanda miti Shule ya Msingi Mahungu kusherehekea siku yao ya kuzaliwa
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Nancy Kivuyo, KIZOTA Watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejumuika pamoja kusherehekea mwezi wa kuzaliwa kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Mahungu. Wakitoa hisia zao za furaha walipotembelea shule hiyo mpya, watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiwemo Afisa Elimu Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mwl. Prisca Mgalula alisema kuwa wameichagua Shule ya Msingi Mahungu ili kuongeza uzuri wa mandhari ya shule hiyo mpya. “Mimi nimezaliwa tarehe 26 Aprili na tumeichagua shule hii kusherehekea kwa kupanda miti takribani 100. Kwa maana hiyo tunaendelea kuhamasisha agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma la ‘Mti wangu, Birthday yangu’ kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kutunza mazingira, lakini pia itawasaidia kujifunzia kwa vitendo hapo baadae" alisema Mwl. Mgalula. Nae, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahungu, Onesphory Massawe alianza kwa kusema kuwa wanafurahi kuwapokea watumushi hao na wanaahidi kuitunza miti hiyo ili ipendezeshe mandhari ya eneo...
Miti 100 yapandwa S/M Mahungu ‘Mti wangu, Birthday yangu’
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, KIZOTA AFISA Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla ameongoza zoezi la upandaji miti 100 katika Shule ya Msingi Mahungu kwa wadau waliozaliwa Mwezi Aprili kwa lengo kuwaandalia mazingira mazuri ya kujisomea wanafunzi shuleni hapo. Alisema kuwa Shule ya Msingi Mahungu ni shule iliyojengwa kwa fedha za serikali kuu kupitia mradi wa Boost awamu ya pili Mwaka wa fedha 2024/2025. Akiongelea zoezi la upandaji miti katika shule hiyo, alisema kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali chini ya kauli hamasishi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ya ‘Mti wangu, Birthday yangu’. “Tupo hapa watumishi tuliojumuika kutoka taasisi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia walimu, wauguzi hadi maaskari. Sisi ni timu ya watumishi waliozaliwa Mwezi Aprili ‘Team Aprili’. Leo tutapanda miti kutekeleza maono ya mkuu wa mkoa kwamba ‘Mti wangu, Birthday yangu’. Kwa hiyo, tutapanda miti 100 katika eneo hili la shule ili kuendelea kukijanisha Dodoma ye...
Ujenzi Ofisi Kata Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Leah Mabalwe, MBALAWALA Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi. Hayo yalizungumzwa na Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella, katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala robo ya tatu 2024/2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema “ninakuagiza Afisa Mtendaji wa kata hii ya Mbalawala kusimamia mradi huu uweze kukamilika kwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanategemea ofisi hii kwaajili ya kupata huduma” alisema Mhandisi Bella. Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Binafsi niishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, kwasababu kazi za maendeleo zinaendelea kufanyika katika kila maeneno na sehemu ambazo hakuna basi Jiji la Dodo...
Wananchi washirikishwe katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago ametoa rai kuwa miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa wananchi washirikishwe kikamilifu ili wawe sehemu ya miradi hiyo na kusema kuwa utaratibu huo utaifanya miradi kudumu kwa muda mrefu. Kauli hiyo aliitoa alipoongoza Kamati ya Fedha na Utawala timu namba tatu kutembelea na kukagua umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Nguji iliyopo Kata ya Ng’hong’onha, jijini Dodoma. Alisema kuwa halmashauri inatekeleza miradi mingi ya maendeleo. “Nitumie nafasi hii kuwasisitiza kuendelea kuwashirikisha wananchi wa eneo husika kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Wananchi wakishirikishwa wanakuwa wamiliki wa mradi husika. Wasiposhirikishwa wanajiona siyo sehemu ya mradi. Hata kama kuna mtu anataka kufanya uharibifu kwenye mradi, wananchi wanabaki wanamtazama kwa sababu hawajashirikishwa. Nitumie nafasi hii kutoa rai, kwenye miradi yetu tunapoitekeleza, tuwashirikishe wananchi ...
Shule mpya ya Kata, Sekondari Miyuji B yajengwa kisasa kutoa elimu bora
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA KAMATI ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imempongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nia yake njema ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora hasa za elimu baada ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo yenye zaidi ya shilingi 500,000,000 katika kata tatu za jiji hilo. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fadhili Chibago alipoongoza timu namba tatu ya Kamati ya Fedha na Utawala kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2024/2025. Alisema kuwa kamati yake ilitembelea kata tatu za Ng’hong’ohna, Makole na Miyuji kukagua miradi ya maendeleo. “Leo tumekuwa na ziara nzuri ya kutembelea miradi mbalimbali katika kata tatu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kamati ya Fedha na Utawala tuligawana na kupeana majukumu ya kutembelea miradi ya maendeleo. Timu yangu tumekagua umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Nguji, Kata ya Ng’hong’onha, uje...
Jengo jumuishi la kutolea huduma za Afya Makole lipo katika hatua nzuri ya ujenzi
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Nancy Kivuyo, MAKOLE Mradi wa ujenzi wa jengo jumuishi la kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya Makole wenye zaidi ya shilingi bilioni moja lipo katika hatua nzuri ya utekelezaji wake. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. Salma Gwassa alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Makole kwa Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyotembelea maendeleo ya mradi huo. Alisema kuwa kiasi cha shilingi 750,000,000 kimetolewa na serikali kuu na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma shilingi 289,794,329 zimelipwa kwa mkandarasi kwaajili ya ujenzi huo. Alisema kuwa ujenzi upo katika hatua ya msingi na wanatarajia mradi utakapokamilika wananchi wa Kata ya Viwandani na Jiji la Dodoma kwa ujumla watapata matibabu hapo. “Mradi huu ukikamilika huduma za kliniki za kibingwa ‘speciality clinic’ zitapatikana, huduma za kiutawala zitaboreka na tutapanua wigo wa utoaji wa huduma kwa wagonjw...