Ujenzi Ofisi Kata Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati
Na. Leah Mabalwe, MBALAWALA
Mradi
wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati ili
wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.
Hayo
yalizungumzwa na Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella, katika zoezi
la ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala
robo ya tatu 2024/2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Alisema
“ninakuagiza Afisa Mtendaji wa kata hii ya Mbalawala kusimamia mradi huu uweze
kukamilika kwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanategemea ofisi hii
kwaajili ya kupata huduma” alisema Mhandisi Bella.
Nae, Awadhi
Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa
kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Binafsi
niishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa
usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, kwasababu kazi za maendeleo zinaendelea
kufanyika katika kila maeneno na sehemu ambazo hakuna basi Jiji la Dodoma
linafika katika eneo hilo na kufanya shughuli za maendeleo ikiwa ni ujenzi wa shule,
barabara pamoja na vituo vya afya. Kwa sasa Dodoma ni Jiji ambalo linafanya
maendeleo ya hali ya juu pasipo na miradi ya serikali kuu, halmashauri
inapeleka miradi ili wananchi waweze kunufaika nayo” alisema Abdallah.
Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala umegharimu kiasi cha shilingi 20,000,000, fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
MWISHO
Comments
Post a Comment