Ofisi ya Kata Zuzu yaboreshwa kwaajili ya utoaji huduma bora
Na. Leah Mabalwe, ZUZU
Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelenga kuboresha mazingira bora ya
kufanyia kazi kwa watumishi wa
serikali ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yalibainishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Zuzu, Shakila Mwanyemba, alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ndani ya robo ya tatu 2024/2025 wakati wa ziara iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala katika Kata ya Zuzu.
“Serikali ya awamu ya sita
ilitenga kiasi cha shilingi 15,000,000 kwaajili ya ukarabati wa Ofisi ya Kata
ya Zuzu, ikiwa ni chachu ya kuboresha mazingira bora kwaajili ya watumishi ili
waweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Pia ofisi hii siyo tu kwaajili ya watumishi
pekee, bali hata wananchi wanaweza kuja kupata huduma bora katika ofisi hii
kutokana na mazingira ya ofisi kuwa bora, salama na rafiki” alisema Mwanyemba.
Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendelea kuboresha utawala bora na kuwasogezea wananchi huduma katika maeneo yao. “Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwasogezea huduma bora wananchi wake ikiwemo huduma za kijamii kama vile ujenzi wa shule, ujenzi wa barabara, vituo vya afya pamoja na kujenga ofisi za kata ili wananchi waweze kupata huduma za kijamii karibu na maeneo yao ya kuishi. Kwahiyo, nitoe pongezi kwa serikali pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuendelea kuratibu na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi” alisema Abdallah.
MWISHO
Comments
Post a Comment