Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma lapongezwa kwa kuimarisha mazingira ya uwekezaji

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA

Sekta ya Biashara na Uwekezaji Wilaya ya Dodoma imepongezwa kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji wa shughuli za kiuchumi, hatua iliyochochea ongezeko la wafanyabiashara na wawekezaji wanaotumia fursa zilizopo kukuza uchumi wa wilaya hiyo.



Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri jijini Dodoma.

Alilipongeza baraza hilo kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika kuhamasisha uwekezaji na shughuli za kiuchumi. “Jiji letu limeendelea kusimamia mifumo inayotoa huduma kwa wananchi. Tunaelezwa kuwa pale SGR huduma ya ‘shuttle’ inapatikana ambapo zinapunguza kadhia kwa wageni ambao hawaujui usafiri wa bajaj na bodaboda. Pia Kanda zimeanzishwa na zinafanya vizuri sana kwa kusaidia wananchi kupata huduma zinazopatikana katika ofisi kuu, hali inayowasaidia kuepuka kupoteza muda na gharama zisizo za lazima. Hapa leo tunawazungumzia wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji ambao ndio tunataka baraza hili liwasimamie ili mazingira ya upatikanaji huduma uwe rafiki na hatimae tunafahamu utasisimua uchumi wa jiji letu” alisema Alhaj Shekimweri.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa uanzishwaji wa One Stop Business Centre ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara kwa urahisi zaidi. Aliongeza kuwa ni muhimu Jiji la Dodoma kupewa nafasi ya uratibu pekee wa kituo hicho huku wafanyabiashara wakisimamia moja kwa moja masuala yao, hatua itakayoongeza ufanisi na uwajibikaji.

Naye mjumbe kutoka sekta binafsi anayewakilisha Chemba ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Tanzania (TNCC), Idd Senge alisisitiza umuhimu wa baraza hilo kuendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kukutana mara kwa mara ili kujadili changamoto na fursa zilizopo. Alisema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha huduma zote muhimu zinazohitajika zinapatikana kwa wakati na kuifanya Dodoma kuwa na mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji.






 

Comments

Popular Posts

SERIKALI YAPONGEZWA KUTOA FEDHA UJENZI WA DODOMA ENGLISH MEDIUM

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma

Nanenane ni muhimu kujifunza Kilimo na Ufugaji bora