DIWANI KATA YA MNADANI ASHIRIKI KIKAO CHA WAZAZI MIYUJI SEKONDARI

Diwani wa Kata ya Mnadani, Mugendi Kerenge amepata wasaa wa kuzungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Miyuji.



Katika kikao hicho Diwani Kerenge alisisitiza umuhimu wa wazazi kushirikiana na walimu katika kusimamia watoto ili kuongeza ufaulu shuleni hapo. Pia alisisitiza kuendeleza uwazi dhidi ya michango ya wazazi wanayotoa katika shule hiyo.

Alitoa wito kwa wazazi na walimu kuhakikisha watoto wote wanapata chakula shuleni chenye virutubisho ili kuongeza uwezo wa kusoma vizuri wakati wote wanapokuwa shuleni.

Diwani Kerenge aliwashauri wazazi kuhakikisha watoto wote wanakaa kambi hasa madarasa ya mitihani ili wapate muda wa kusoma vizuri.

 

Comments

Popular Posts

Prof. Mohamed ahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwapongeza wazazi

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni nyenzo ya utendaji kazi serikalini – Dkt. Biteko

Mamia wajitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru 2026 Kata ya Kikuyu Kusini