OCPD yapongeza ushirikiano na Ofisi ya Mashitaka katika zoezi la Urekebu wa Sheria
Na. Calvin Gwabara, DODOMA
Ofisi
ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imekabidhi Juzuu za toleo la Urekebu wa
Sheria la Mwaka 2023 kwa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na kupongeza mchango
mkubwa uliotolewa na Ofisi hiyo kupitia watumishi wake kwenye utekelezaji wa
zoezi la Urekebu.
“Wakati tunaanza zoezi hili Ofisi yetu ilikuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa watumishi hasa Mawakili wa kufanya kazi hii lakini tulikuwa tukibisha hodi kwenye Ofisi yako kuomba Mawakili kuja kushirikiana nasi katika kutekeleza zoezi hili, na hakika walitusaidia sana hadi tumekamilisha” alieleza Katuga.
Aliongeza
“Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa kutambua mchango wenu imeona ni muhimu
na Ofisi yako pia ipate nakala hizi ingawa tunatambua kuwa tumeleta chache
kutokana na gharama lakini ziwasaidie kwa kuanzia na kuwa kama kumbukumbu
kwenu, lakini mnaweza kupata nakala laini zote kupitia mfumo wa OAG MIS
library” alieleza Katuga.
Kaimu
Mkurugenzi huyo wa Divisheni ya Urekebu, Tafiti na Mafunzo ameongeza kuwa
pamoja na nakala hizo tano pia wameipatia Ofisi hiyo tuzo maalumu kutoka Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kutambua mchango wa Ofisi ya Taifa
ya Mashitaka katika zoezi hilo la Urekebu wa Sheria.
Akizungumza
kwa niaba ya watumishi wa Ofisi yake Mkurugenzi wa Mashitaka, Sylvester
Mwakitalu alipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) na kushukuru kwa
kuwapatia nakala hizo za kuanzia kwaajili ya Ofisi yake maana wangeenda kununua
dukani ingekuwa gharama kubwa.
“Ofisi yetu tunatumia Sheria hizi kila siku maana tunatoa huduma za mashitaka kwenye mahakama zote nchini hasa hasa Mahakama za Wilaya na za Hakimu Mkazi ndiko tunaenda huko kila siku, lakini pia Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa. Kwahiyo, hizi Sheria ni nyenzo muhimu sana kwetu” alieleza Mwakitalu.
Aliongeza
“nakala hizi tulizozipata tutazisambaza kwa Mawakili wetu kwanza, alafu sisi
tutaendela kusubiria kupata zingine kwa utaratibu maalumu lakini pia kwa
kutumia zle ambazo zinazopatikana kwenye mfumo kwa nakala tepe”.
Toleo
la Urekebu wa Sheria la Mwaka 2023 lilizinduliwa na kwa mujibu wa Sheria na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mwezi Aprili, Mwaka
huu na kutangaza kuanza kutumika tarehe 1/07/2025 na hivyo kufuta Toleo la Sheria
la Mwaka 2002.
Chanzo:
Michuzi Blog
Comments
Post a Comment