BAgamoyo Garden kuipendezesha Dodoma

 

Na. Mwandishi wetu,

MRADI wa Bagamoyo Garden wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi unalenga kuunga mkono juhudi za serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani na inayopendeza.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa mradi wa Bagamoyo Garden, Rogasian Malya alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa Bagamoyo Garden wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi katika eneo la wazi kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024.

Malya alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa njia ya upandaji miti, kampeni ambayo ilizinduliwa mwaka 2021 kwa kupanda miti katika chanzo cha maji Mzakwe na aliyekuwa Makamu wa Rais ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisema kuwa mradi huo unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru, 2024 usemao Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu. Mradi umefanikiwa kuzalisha na kuuza jumla ya miche 1,590,000 kwa wadau mbalimbali. “Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi 25,700,000.00 ikijumuisha gharama za usafishaji wa eneo, uwekaji wa miundombinu ya maji, ununuzi wa malighafi za ujenzi kwa ajili ya utengenezaji wa vyungu, sanamu za wanyama na malipo ya wafanyakazi” alisema Malya.

Mradi wa Bagamoyo Garden ulianza tarehe 21 Desemba, 2022 ukiwa umeajiri vijana 20 kwa ajira ya muda mfupi katika eneo lenye ukubwa wa mita mraba 3,600 likiwa na miti mbalimbali iliyo tayari kwa matumizi.

MWISHO


Comments

Popular Posts

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Waziri Mchengerwa apongeza usimamizi wa miradi jijini Dodoma

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma