Barabara ya Judiciary kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dodoma
Na. Dennis Gondwe, TAMBUKARELI
UJENZI wa barabara ya ‘Judiciary’
yenye urefu wa kilometa mbili unalenga kupunguza msongamano wa magari katikati
ya Jiji la Dodoma na kuharakisha huduma kwa wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja
wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya
ya Dodoma, Mhandisi Emmanuel Mfinanga wakati akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi
wa barabara ya Judiciary yenye urefu wa kilometa mbili kwa kiongozi wa mbio za Mwenge
wa Uhuru kitaifa.
Mhandisi Mfinanga
alisema ”ndugu kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2024, lengo
la mradi huu ni kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dodoma,
kurahisisha huduma kwa wananchi katika ofisi zilizopo katika eneo hili ambapo
miongoni mwa ofisi hizo ni:- Ofisi ya Bima (NHIF), Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), Wakala wa Ununuzi Tanzania (PPRA), Ofisi za Maadili ya
Viongozi wa Umma na Ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Mnzava baada ya kuweka jiwe msingi mradi wa barabara ya Judiciary KM 02 |
Alisema kuwa eneo la NCC Link
lina barabara zenye jumla ya kilomita 9.8, barabara ya ’Judiciary’ ni miongoni
mwa barabara hizo. Kutokana na umuhimu wa barabara katika eneo hili, Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ilitenga fedha
kiasi cha shilingi 2,409,187,951.00 kwa ajili ya ujenzi wa Kilomita mbili
za lami ngumu, aliongeza.
Comments
Post a Comment