COSTECH YAFADHILI MIRADI YA UTAFITI KUHUSU SOMO LA HISABATI
Na Janeth Raphael - MichuziTv
- Dodoma.
TUME
ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili miradi miwili wenye
thamani ya Sh.milioni 120 kwa kila mradi kwa lengo la kufanya utafiti katika
somo la hisabati kutokana na matokeo mabaya ya somo hilo katika mtihani wa
darasa la saba na kidato cha nne.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt.Amos Nungu
Akizungumza
leo Agosti 25,2023 na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa
COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema imeidhinisha miradi miwili kwa
thamani ya Sh.milioni 120 kila mradi na utekelezaji wa mradi unahusisha
watafiti kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini.
Amefafanua
mradi utafanyika katika kipindi cha miaka miwili na hatua iliyopo sasa ni
kusaini mikataba. "Somo la hisabati bado ni changamoto kwani matokeo yake
yamekuwa mabaya kwa kidato cha nne na darasa la saba.
"
Hivyo kwa kuondoa tatizo hilo Tume tumeidhinisha miradi miwili ambayo
kila mmoja thamani yake ni Sh.milioni 120,"amesema na kuongeza miradi
mingi ya utafiti hufadhiliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu.
"Kwa
sasa ipo miradi kadha inayoendelea na ipo hatua mbalimbali ambayo Serikali
ilifadhili kupitia COSTECH. Michache katika miradi hiyo ya utafiti inayoendelea
katika hatua mbalimbali za utekelezaji, " amesema.
Ameongeza
kwamba na Tume inafanya ufuatiliaji ikiwemo ile inayohusu kuboresha maabara za
utafiti kwa ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo.
Pia
amesema katika kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti, baadhi ya shughuli
zilizotekelezwa ni pamoja na kuibua na kufadhili miradi ya kimkakati ambayo
michakato imefanyika tayari na sasa ipo hatua ya mikataba ikiwemo kuyaelewa na
kuyatumia vema mapinduzi ya nne ya Viwanda ndiyo mwelekeo kwa dunia nzima.
Dkt. Nungu
amesema Serikali kupitia COSTECH imeidhinisha jumla ya miradi saba kwa thamani
ya Sh.milioni 150 kila mradi. Miradi hiyo itafanyika ndani ya miaka
miwili na inahusisha watafiti na wabunifu kutoka sekta zote umma na binafsi.
Amesema
COSTECH inaendelea kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuanzisha au kutoa
usaidizi kwa vituo mbalimbali vya ubunifu (intemediaries) ili kuwafikia na
kuwahuduma wabunifu kiurahisi.
Pia
kuweka mazingira wezeshi kwa ujumla wake katika ubunifu ni pamoja na kuwa na
mfumo stahiki inayosaidia wabunifu na bunifu nchini."Tumekuwa na kumbi za
ubunifu , kuwapokea na kuwalea wabunifu, Sera na miongozo, mitaji."
CHANZO: Michuzi Blog
Comments
Post a Comment