MENEJIMENTI YA TANESCO YARIDHISHWA NA UJENZI WA MRADI WA BWAWA LA KUFUA UMEME WA JULIUS NYERERE (JNHPP)
Na Neema Mbuja, Rufiji
Timu ya Menejimenti ya Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) imetembelea mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP
huku ikieleza madhumuni ya ziara hiyo ikiwemo kufanya tathimini ya mwenendo wa
ujenzi wa mradi unaokaribia asilimia 91 ifikapo Agosti mwishoni.
Lengo jingine la ziara hiyo ni
kuangalia mwenendo wa ujenzi wa mradi na tathimini ya hali ya mvua za vuli
zinazotarajiwa kunyesha kati ya Oktoba hadi Disemba kama ilivyotangazwa na
Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Timu hiyo imeongozwa na Mkurugenzi
mkuu wa Tanesco Maharage Chande.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Chande amesema maendeleo ni mazuri hadi Julai tulifikia asilimia 90 na
tunatarajia mwishoni mwa Agosti tutafikia asilimia 91 huku akiwapongeza
wahandisi na wafanyakazi wa shirika hilo wanaosimamia mradi huo.
Amesema ukamilikaji wa mradi
huu utatuwezesha kushinda mashindano haya kwa kuwa na umeme wa uhakika
utakaokidhi mahitaji ya uchumi. Amesema timu ya menejimenti ya Tanesco imani
kukamilika mradi huo utakuwa na mchango mkubwa wa kuondoa cngamoto ya upungufu
wa umeme unaojitokeza katika miezi ya Oktoba na Desemba.
“Mambo yanakwenda na huenda
upungufu wa umeme ukawa historia huko tunakokwenda, tutaongeza umakini katika
utekelezaji wake,” amesema Maharage.
Kwa mujibu wa Chande kumekuwa
na ongezeko la mahitaji ya umeme hafi kufikia megawati 1,482.7 mwezi huu kutoka
megawati 1,354 za mwaka 2022.
Ameifananisha hatua hiyo na
mashindano makubwa ya kutumia umeme kutokana na mahitaji huku Tanesco ikiongeza
uzalishaji ili kukidhi mahitaji kwa Watanzania.
Hali kadhalika pia Chande
amesema timu ya menejimenti ya Tanesco imetembelea mradi huo kwa ajili ya
kufanya tathimini kuhusu mvua zitakazonyesha miezi inayokuja.
” Endapo utabiri huo utakwenda
kama ulivyopangwa basi bwawa hilo litajaa kwa haraka zaidi.Zikinyesha kama
ilivyotarajiwa itakuwa heri, lakini zikiongezeka tumejiandaa kwa kuweka mipango
itakayohakikisha kazi za mradi zinaendelea pasipo kupata changamoto,
Katika kuwaanda mapema
wataalamu watakaoendesha mradi huo, Maharage amesema tayari wameshaongeza
wafanyakazi zaidi ya 24 kwa ajili ya kujiandaa kuendesha mchakato huo
utakapokamilika.
Amefafanua kuwa ili mradi huo
uanze kufanya kazi unahitaji wafanyakazi 221 watakaouendesha pindi
utakaokamilika, akisema kwa sasa jumla wapo zaidi ya 90 na watakuwa na
wakiwapeleka kwa awamu kulingana na mradi utakapofikia.
Chande amesema jumla watumishi
221 wanahitajika kuendesha mradi huo, lakini hawatapelekwa kwa wakati mmoja,
bali kwa makundi yatakayoenda kwa wakati husika
.Amesema kundi lililopo sasa
hivi linahusika na utalaamu wa uhandisi mitambo ya umeme.
“Kutakuwa na wafanyakazi
madaktari, walimu wa shule za awali, wahasibu. Tutaendelea kuongeza wafanyakazi
kwa makundi kulingana na hatua ya ujenzi wa mradi utakapofikia,
Mkurugenzi wa Fedha wa shirika
hilo, Renatha Ndege amesema menejimenti ya shirika hilo imeamua kutembelea
mradi huo ili kuangalia mwenendo wa utekelezaji wake, akisema ukikamilika Juni
mwakani utakuwa mkombozi mkubwa kwa Watanzania.
Comments
Post a Comment