Na. Mwandishi wetu, DODOMA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi, Wizara na Taasisi zinazohusika na sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kutumia kikamilifu miundombinu, teknolojia na mitaji iliyowekezwa na Serikali ili kuongeza tija na ushindani wa Taifa katika masoko ya ndani na nje. Akizungumza katika kilele cha Maonesho na Sherehe za wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni, Rais Dkt. Samia amesema miradi ya umwagiliaji iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa inapaswa kusimamiwa kwa viwango bora ili kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji na kukuza tija ya mavuno. Alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti ya kilimo ili kugharamia ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji, mabwawa na visima, pamoja na kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja, huku upatikanaji wa mbegu bora na mbolea ya kisasa ukiimarika kupitia ruzuku na kuanzishwa kwa viwanda vya uzalishaji, hatua iliyo...
Comments
Post a Comment