TRA YAZINDUA KAMPENI KUELEZEA UMUHIMU RISITI ZA MASHINE ZA EFD

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Husna Nyange amesema kodi sahihi inatokana na kumbukumbu sahihi za kikodi hivyo amewahimiza wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapofanya mauzo.




Pia na wanunuzi kudai risiti sahihi za EFD kila wanaponunua bidhaa au kupata huduma lengo likiwa kila mmoja kwa nafasi yake anatunza kumbukumbu zake.

Nyange ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mabango ya uhamasishaji kuhusu matumizi sahihi ya EFD.

Hivyo pamoja na mambo mengine ameelezea umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na kumbukumbu sahihi za kikodi hivyo lakini wanunuzi nao ni vema wakajenga utamaduni wa kudai risiti kutoka kwa wafanyabiashara.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Huduma kwa Mlipakodi Mkoa wa kikodi Kinondoni Emanuel Lucian Dafay amesema kampeni hiyo ya EFD ni endelevu na kwa mkoa wa Kinondoni walianza kwa kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa wafanyabiashara kupitia simu zao za mkononi.

Amefafanu lengo la kutuma ujumbe ili kuwakumbusha kuhusu wajibu wao wa kutoa risiti sahihi za EFD. “Wafanyabiashara wa Mkoa wetu wa Kinondoni wamepata meseji za kuwakumbusha umuhimu wa kutoa risiti" amesema.

Wakati huo huo wafanyabiashara wameipongeza TRA kwa kuendelea kuwakumbusha wajibu wao kuhusu mambo mbalimbali ya kikodi ikiwemo kutoa na kudai risiti.

Pia wafanyabiashara wamehaidi kutimiza wajibu wao wa kutoa risiti kila watakapofanya mauzo.




 

CHANZO: Michuzi Blog

Comments

Popular Posts

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Waziri Mchengerwa apongeza usimamizi wa miradi jijini Dodoma

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma