Posts

RC Senyamule aagiza utengenezaji Viti uende sambamba na ujenzi wa madarasa Sekondari Mtumba

Na. Dennis Gondwe, MTUMBA MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza ujenzi wa madarasa uende sambamba ya utengenezaji wa viti na meza kwa ajili ya wanafunzi ili vyote vikamilike pamoja na kuanza kutoa huduma. Kauli hiyo aliitoa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Mtumba iliyopo Kata ya Mtumba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Baada ya kukagua hatua ya ujenzi wa miundombinu hiyo alihoji hatua ya utengenezaji wa viti na meza ambao ulikuwa haujaanza. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliagiza utaratibu wa kutengeneza viti na meza uanze ili uende sambamba ya ujenzi wa miundombinu hiyo na kukamilika pamoja ili isicheleweshe utoaji wa huduma. Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 10 ya vyoo kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2024/2025 Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtumba, Mwl. Stephen Moshi alisema kuwa ujenzi unaendelea vizuri. “Shule ilipokea shilingi 201,000,000 tarehe 6 Ja...

RC Dodoma afurahishwa ujenzi Sekondari Mtemi Chiloloma

Na. Dennis Gondwe, HOMBOLO MAKULU MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameagiza ujenzi wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma kusimamiwa vizuri ili ukamilike katika muda uliopangwa kwa ajili ya kutoa huduma. Agizo hilo alilitoa alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Kata ya Hombolo Makulu, jijini Dodoma. Awali akikagua ujenzi huo alieleza kufurahishwa kwake na hatua ya ujenzi wa shule hiyo. Aliwataka viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusimamia vizuri mradi huo ili uweze kukamilika katika muda uliopangwa. Akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba nane vya madarasa na matundu 18 ya vyoo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtemi Chiloloma, Mwl. Livinus Tanganyika alisema shule yake ilipokea shilingi 216,000,000 kutoka serikali kuu. “Ujenzi ulianza tarehe 25 Novemba, 2023 mpaka sasa ujenzi wa madarasa umekamilika kwa asilimia 100, matundu ya vyoo 18 yapo hatua ya umaliziaji, kazi inayoendelea ni kuweka mar...

Matukio katika picha ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo kipindi cha robo ya tatu mwaka 2023/2024

Matukio katika picha ziara ya Kamati ya Fedha na Utawala kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo kipindi cha robo ya tatu mwaka 2023/2024

Matukio katika picha zoezi la kupanda miti Shule ya Msingi Amani na Dodoma Mlimani kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania lilifanywa na Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Jiji la Dodoma

Image
 

Matukio katika picha zoezi la usafi wa Mazingira Kituo cha Afya Makole kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano lililofanywa na Divisheni ya Elimu Sekondari Jiji la Dodoma

Image
 

Elimu Sekondari yafanya usafi Kituo cha Afya Makole

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA DIVISHENI ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeadhimisha maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya usafi katika Kituo cha Afya Makole kwa lengo la kuwawekea mazingira safi na salama wagonjwa wanaopata huduma kituoni hapo. Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Zainabu Abdallah akiongea na mamia ya walimu, wanafunzi na Jumuiya ya Kituo cha Afya Makole Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Zainabu Abdallah alipokuwa akiongea na mamia ya walimu, wanafunzi na jumuiya ya wafanyakazi wa Kituo cha Afya Makole kufanya usafi katika kituo hicho. Mwl. Abdallah alisema “sisi Divisheni ya Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma tumeamua kuadhimisha maadhimisho ya kuelekea miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya usafi katika Kituo cha Afya Makole. Kama mnavyofahamu Makole ni kituo cha ...

Matukio Dua na Sala ya Kitaifa kuliombea Taifa la Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Dodoma

Image
 

Midahalo ya kupinga rushwa kupunguza kero kwenye jamii

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri anaendesha midahalo ya kupinga rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na kuhamasisha haki za binadamu na utawala bora ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri Hayo yalibainishwa wakati wa salamu za mkuu huyo wa wilaya kwenye hafla ya ufunguzi wa mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar, Kisasa jijini Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema kuwa zipo haki za watu ambazo zinapotea kwa sababu na rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na ukatili dhidi ya watoto. “Kwa maelekezo ya mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba tushughulikie kero na tunamshukuru mkuu wa mkoa ametuongoza tumeanzisha kampeni katika mkoa wake ya ‘ kero yako, wajibu wang...

Tume ya Haki za Binadamu yasisitiza utawala bora

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA TUME ya Haki za Binadamu na Utawala bora ina dhamira kuona watanzania wanaheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na utu wa mtu. Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Dkt. Thomas Masanja Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, Dkt. Thomas Masanja alipokuwa akitoa salamu za tume hiyo katika hafla ya kufungua mashindano ya mdahalo kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kuhusu madhara ya rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, haki za binadamu na utawala bora katika ukumbi wa St. Gaspar Kisasa jijini Dodoma. Dkt. Masanja alisema “tunashiriki katika shughuli hii inayohusisha wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kwa sababu dira ya tume ni kuona jamii yenye utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na utu wa mtu. Tunataka mwisho wa siku jamii ya kitanzania inaheshimu haki za binadamu, utu wa mtu na misingi ya utawala bora”. Akiongelea ushir...