Dodoma Jiji yaangukia pua dhidi ya Ujenzi Queens Mwenge Super Cup

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

TIMU ya Mpira wa Pete ya Wizara ya Ujenzi (Ujenzi Queens) imeibuka kidedea kwa kuifunga Timu ya Mpira wa Pete ya Dodoma Jiji kwa magoli 37-33 katika mchezo wa kuvutia uliochezwa katika viwanja vya Chinangali Park.


Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida na kuendelea kushika kasi kadri muda ulivyokuwa ukisogea.

Hadi mchezo unamalizika, Timu ya Ujenzi Queens iliikuba na ushindi wa magoli 37 dhidi ya 33 ya Dodoma Jiji.

Awali Kocha wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ujenzi Queens Mwamvita Mzee alisema kuwa wamekuwa wakipata matokeo mazuri kutokana na kufanya mazoezi mara kwa mara. “Timu yetu inaamini katika mazoezi ya mara kwa mara. Kama unavyofahamu mazoezi hayadanganyi, tumekuwa tukifanya mazoezi kwa bidii ndiyo siri ya mafanikio yetu. Zidi ni kupendana kama timu na watu kujitoa kwa ajili ya timu na kuupenda mchezo. Pia, kwetu ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Tanzania ya kufanya mazoezi kwa watumishi mahala pa kazi” alisema Mzee.

 

Kwa upande wake Afisa Michezo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Neema Kilongola alisema kuwa mashindano ya Mwenge Super Cup Mwaka 2026 yanalenga kuwahamasisha wanamichezo na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma.






MWISHO

Comments

Popular Posts

Afisa Elimu Jiji la Dodoma anunua jina la Rais Samia kwa Laki 5