Hazina Volleyball yaiduwaza Dodoma Jiji Seti 2-0 Mwenge Super Cup


Na. Dennis Gondwe, DODOMA

TIMU ya Wanaume ya Mpira wa Mikono ya Hazina (Hazina Volleyball Club) imeibuka na ushindi wa Seti 2-0 dhidi ya Timu ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa katika viwanja vya Chinangali Park mapema leo.


Akiongelea mchezo huo, Nahodha wa Timu ya Hazina Volleyball Club, George Kalunde alisema timu yake ilijiandaa vizuri kuelekea mchezo huo ndio sababu ya kupata ushindi wa Seti 2-0.

Aidha, aliipongeza Wilaya ya Dodoma kwa kuandaa mashindano ya Mwenge Super Cup Mwaka 2026 na kutaja maandalizi hayo kuwa ni ubunifu mkubwa. “Nitumie nafasi hii kuwahamasisha vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma, karibuni sana.

Nae Nahodha wa Timu ya Mpira wa Mikono ya Dodoma Jiji, Muhidin Mwenda alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri pamoja na kufugwa. “Tunapenda kumshukuru Mungu tumemaliza mechi salama, pamoja na kuwa tumepoteza mechi kwa seti 2-0, siyo matokeo mazuri kwetu. Mashindano haya yamekuwa chachu kwa ajili ya kuimarisha mwili lakini yamekuwa hamasa kwa ajili ya maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru siku chache zijazo. Kaulimbiu isemayo Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo imetutia hamasa zaidi na tunajiona ni sehemu ya kuhamasisha amani na maendeleo” alisema Mwenda.





MWISHO

Comments

Popular Posts

Maafisa Biashara wa Morogoro na Ruvuma watembelea Banda ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya Sabasaba, 2026

Msalato wamshukuru Rais, Dkt. Samia ujenzi wa shule

Hakuna Mamluki yeyote atakayeandikishwa kwenye orodha ya wapiga kura Jiji la Dodoma