Ujenzi wa Madarasa ya kisasa wavutia wanafunzi kusoma kwa bidii Sekondari Kikuyu
Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kikuyu, Mwl. Gasper Mmary amesema mradi wa ujenzi wa
madarasa ya kisasa umekuwa chachu ya ufaulu na kuvutia wanafunzi kusoma kwa
bidii.
Alisema
kuwa anaishukuru serikali kwa kutoa kiasi cha shilingi 40,000,000 kwaajili ya
ujenzi wa madarasa mawili ya kisasa na ofisi moja ya walimu. “Tunaishukuru sana
serikali ya awamu ya sita, ujenzi huu wa madarasa ya kisasa umesaidia sana
katika kupanda kwa taaluma kwa wanafunzi wetu na hata kupanda daraja la ufaulu.
Madarasa haya yanawavutia wanafunzi kukaa kwa muda mrefu shuleni kwaajili ya
kujisomea na mazingira kwa ujumla ni mazuri” alisema Mwl. Mmary.
Kwa
upande wake Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Kikuyu, Mwl. Mwajuma Kidela aliipongeza
serikali kwa kujenga madarasa kwasababu yameleta mchango mkubwa sana katika
kujifunza kwa wanafunzi. Alisema kuwa wanafunzi hawana uhaba wa madarasa baada
ya serikali kuboresha zaidi sekta ya elimu. “Kwa hivi sasa madarasa yapo na
yanakidhi viwango, wanafunzi wanakaa kwa nafasi hasa wanapokuwa darasani” alisema
Mwl. Kidela.
Nae,
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikuyu, Conjester Mwanika alimshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa madarasa katika shule yao. “Kabla
ya ujenzi huu wa madarasa katika shule yetu, hapo awali tulikuwa tukipata shida,
madarasa yalikuwa hayatoshelezi na wanafunzi tulikuwa tukikaa kwa kujibana na
hiyo ilikuwa ikimuwia vigumu mwalimu kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja. Lakini
kwa hivi sasa tunamshukuru Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuona na
kusababisha hata ufaulu kuongezeka katika shule yetu” alisema Mwanika.
MWISHO
Comments
Post a Comment