TAMISEMI yakusanya Shilingi Trilioni 1.11
OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema hadi kufikia Machi, 2025 shilingi trilioni
1.11 zimekusanywa sawa na asilimia 93.15 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni
1.60 kwa Mwaka 2024/25.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa
Akiwasilisha bungeni makadirio ya
mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2025/26, Waziri Mchengerwa alisema
kuwa kati ya fedha hizo shilingi trilioni 61.21 ni kodi ya majengo, shilingi trilioni
1.04 ni mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa.
Pia, alisema kuwa shilingi bilioni
16.23 ni mapato ya ndani ya taasisi na shilingi milioni 201.60 ni maduhuli ya
mikoa.
Alifafanua kuwa makusanyo hayo
yalitokana na ada za wanachuo, tozo, ukusanyaji wa madeni, mauzo ya bidhaa
mbalimbali na ushuru unaotozwa na mamlaka za serikali za mitaa kulingana na
Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290.
Mchengerwa alisema kuwa kwa kipindi
hicho, TAMISEMI ilipanga kutumia shilingi bilioni 541.27 za mapato ya ndani ya
halmashauri kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hadi kufikia
Machi, 2025 shilingi bilioni 312.30 sawa na asilimia 57.70 zilitolewa.
Alielezea kuwa baadhi ya miradi
iliyotekelezwa kwa kipindi hicho ni ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya,
ujenzi wa barabara, machinjio, minada nyumba za walimu na watumishi wa afya,
hospitali, vituo vya afya, zahanati, vituo vya polisi, ununuzi wa magreda.
Chanzo: www.tamisemi.go.tz
Comments
Post a Comment