Bagamoyo Garden yaajiri vijana 20 Dodoma
Na. Dennis Gondwe
MRADI wa Bagamoyo Garden wa utunzaji na uhifadhi wa
mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi unalenga kuunga mkono juhudi
za serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani na inayopendeza.
Sehemu ya muonekano wa Bagamoyo Garden
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa mradi wa Bagamoyo
Garden, Rogasian Malya alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa Bagamoyo Garden wa
utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, maua na nyasi
katika eneo la wazi kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024.
Malya alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuunga
mkono juhudi za serikali
za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa njia ya upandaji miti, kampeni ambayo ilizinduliwa mwaka
2021 kwa kupanda miti katika chanzo cha maji Mzakwe na aliyekuwa Makamu wa Rais
ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan. Alisema kuwa mradi huo
unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mbio
za Mwenge wa Uhuru, 2024 usemao ‘Tunza
Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa endelevu’. Mradi umefanikiwa kuzalisha na kuuza jumla ya miche
1,590,000 kwa wadau mbalimbali. “Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, mradi huu umegharimu kiasi
cha shilingi 25,700,000.00 ikijumuisha gharama za usafishaji wa eneo, uwekaji wa
miundombinu ya maji, ununuzi wa malighafi za ujenzi kwa ajili ya utengenezaji
wa vyungu, sanamu za wanyama na malipo ya wafanyakazi” alisema Malya.
Mradi wa Bagamoyo Garden ulianza
tarehe 21 Desemba, 2022 ukiwa umeajiri vijana 20 kwa ajira ya muda mfupi katika
eneo lenye ukubwa wa mita mraba 3,600 likiwa na miti mbalimbali iliyo tayari
kwa matumizi.
MWISHO
Comments
Post a Comment