Dodoma Media Group
Na. Dennis Gondwe, MIYUJI
Kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group
kutoa elimu ya mpiga kura katika kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na
utunzaji wa mazingira.
Mejena Mkuu wa Dodoma Media Group, Zania Miraji alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group
Kauli hiyo ilitolewa na Mejena Mkuu wa Dodoma Media Group,
Zania Miraji alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa kituo cha vyombo vya habari
cha Dodoma Media Group kilichopo katika Mtaa wa Miyuji Proper jijini Dodoma kwa
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024.
Miraji alisema “kupitia vyombo vya habari vya Dodoma Media Group
jamii ya Dodoma itapata haki ya upatikanaji wa taarifa na elimu juu ya masuala
mbalimbali ikizingatia ujumbe
wa ‘Tunza Mazingira na
Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi
wa Taifa Endelevu’. Elimu itakayotolewa ni pamoja na elimu ya masuala ya uchaguzi ikiwemo
elimu ya mpiga kura ambapo kutakuwa na kipindi maalum cha kuelimisha Umma
kujiandaa na uchaguzi wa serikali
za mitaa. Pia itatolewa elimu juu ya lishe na kutakuwa
na kipindi maalum kitakachozungumzia masuala ya lishe na elimu juu ya utunzaji
wa mazingira na athari za uharibifu wa mazingira”.
Akiongelea
lengo la mradi huo alisema kuwa ni kiunganishi muhimu kati ya sekta binafsi,
serikali na jamii. Aliongeza kuwa mradi unaunga mkono jitihada za serikali chini ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamishia shughuli
za serikali na sekta binafsi mkoani Dodoma. “Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru Kitaifa 2024, mradi huu ukikamilika utatoa ajira kwa wafanyakazi 36
kati yao Wanaume 19 na wanawake 17 miongoni mwao watu wenye Ulemavu ni 03”
alisema Miraji.
Akiongelea
gharama za mradi, alisema kuwa hadi kukamilika utagharimu shilingi
1,000,000,000. Alisema kuwa hatua iliyofikiwa kiasi cha shilingi 700,000,000
kimetumika sawa na asilimia 70, akivitaja vyanzo vya fedha kuwa ni matangazo ya
biashara, mkopo na mapato binafsi ya mkurugenzi.
Mradi wa kituo cha vyombo vya habari cha Dodoma Media Group
ulianza kutekelezwa tarehe 1 Oktoba, 2018 ukitarajiwa kukamilika tarehe 31
Desemba, 2024, ukihusisha ujenzi wa majengo ya studio za redio, televisheni,
samani na mifumo ya umeme na maji.
MWISHO
Comments
Post a Comment