TTB NI NGUZO YA KUTANGAZA UTALII
Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Bodi ya Utalii (TTB) ndiyo nguzo muhimu katika
kutangaza na kuvutia watalii kutembelea Nchi yetu sanjari na kuongeza mapato
yatokanayo na Sekta ya Utalii.
Mhe.
Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Bodi za Wakurugenzi za TTB
na Hifadhi ya Taifa (TANAPA) uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa AICC jijini Arusha na kuitaka TTB kuanza mikakati ya kubaini fursa za
uwekezaji kwenye utalii.
Amesema
kuwa Serikali ipo katika kufanya mapitio ya sheria ambayo itawapa mamlaka TTB
kuhakikisha kwamba wanaishauri vyema kwenye eneo la uwekezaji kwenye sekta ya
utalii.
“TTB
mtakuwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kuna nyongeza ya ujenzi wa hoteli
mbalimbali, nyongeza ya vyumba na kufikiria kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali
ya ufukwe au kwenye visiwa” amesema Mhe Mchengerwa
Amesema
kuwa kwenye suala la uwekezaji wanatambua hadi leo hii idadi ya vyumba
vilivyopo nchini kwa ajili ya watalii ni ndogo sana ambavyo ni 120,000
ukilinganisha na nchi jirani ya Kenya yenye vyumba zaidi ya milioni 1,500,000.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Dkt Mohamed Dau amemshukuru Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani
aliyoionesha na kumpa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB.
Dkt.
Dau amesema kuwa takwimu zinaonesha bara la Asia ndilo lina watu wengi ambapo
kunahitaji kuweka mkazo wakutangaza Utalii kwenye Bara la hilo kwasababu huko
ndiko watalii wengi wapo ili kuweza kuongeza idadi ya watalii kuja Tanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bw. Damasi Mfugale amesema TTB itaendelea
kubuni mikakakati mbalimbali yenye lengo la kuimarisha uhifadhi, utangazaji na
uendelezaji wa Sekta ya Utalii nchini.
Amesema
kuwa mikakakti hiyo itazingatia mawazo na miongozo itakayotolewa na bodi za
wakurugenzi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ametoa
pongezi kwa Mhe Rais katika kazi kubwa anayoifanya katika kulea uhifadhi na
kutangaza Utalii na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi za Wakurugenzi
zilizoteuliwa ili ziweze kutimiza malengo ya Taifa na Taasisi zao.
Wakati
huo huo, Bodi ya Utalii Tanzania imeaingia makubaliano ya ushirikiano na
Kamisheni ya Utalii Zanzibar ikiwa na lengo la kuongeza ushirikiano wa
kitengaji katika taasisi hizo.
Comments
Post a Comment